Home BUSINESS KUBORESHA MPAKA KATI YA ZAMBIA NA TANZANIA KUDHIBITI UTOROSHWAJI WA BIDHAA

KUBORESHA MPAKA KATI YA ZAMBIA NA TANZANIA KUDHIBITI UTOROSHWAJI WA BIDHAA

Na Chedaiwe Msuya, WF, Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) amesema katika kudhibiti utoroshwaji wa mazao na bidhaa nchini Serikali imeboresha mpaka kati ya Tanzania na Zambia ambapo Mamlaka ya Mapato (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zambia (ZRA) ziliingia makubaliano (MoU) yenye lengo la kuchukua hatua mbalimbali za kulinda utoroshwaji huo.
 
Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakati akijibu swali la Mbunge wa Mhe. Condester Sichalwe (MOMBA), aliyetaka kujua ni lini Serikali itaboresha mpaka ya zambia na Tanzania ili kudhibiti njia za panya ambazo mazao na bidhaa hutoroshwa bila kulipiwa kodi.
 
Mhe. Chande, alisema ZRA na TRA zimeingia makubaliano ya kuboresha mfumo wa uondoshaji mizigo TANCIS ambapo umeunganishwa na mfumo wa ASYCUDA World wa Zambia ili kubadilishana taarifa na kurahisisha taratibu za uondoshaji mizigo.
 
“Serikali pia imesimika midaki (baggage and cargo scanners) za kukagua mizigo inayobebwa na abiria pamoja na magari”,Alisema Mhe. Chande
 
Aidha, aliongeza kuwa Serikali ya Zambia pia inapanua barabara na eneo la maegesho ya upande wa Nakonde ili kupunguza msongamano upande wa Tunduma.
 
Pia,alisema kuwa Serikali inaendelea kubainisha vihatarishi vilivyopo katika magari ya mizigo yanayopita mpaka wa Tanzania na Zambia.
 
Sambamba na hayo, Mhe. Chande alisema pamoja na hatua hizo kuchukuliwa pia Serikali kupitia TRA inaendelea kuimarisha doria kwa ajili ya kudhibiti maeneo yote ya mpaka wa Tanzania na Zambia kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kulinda mapato ya serikali.

Previous articleSOMA MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNI 25-2024
Next articleMBUNGE MTATURU ASISITIZA MAMBO MANNE KWA SERIKALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here