Home LOCAL KITUO CHA POLISI MKIWA KUKAMILIKA

KITUO CHA POLISI MKIWA KUKAMILIKA

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameihoji serikali ni lini itaunga mkono jitihada za wananchi,wadau na Mbunge kupitia mfuko wa Jimbo katika ujenzi wa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Kata ya Mkiwa ili kituo hicho kikamilike na kisaidie kuimarisha usalama wa wananchi.

Mtaturu ameuliza swali hilo Juni 12,2024,Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu.

“Kata ya Mkiwa tumeanza ujenzi wa kituo kidogo cha polisi ambacho ni kituo cha mkakati ,mimi kama Mbunge kupitia Mfuko wa Jimbo nimechangia Milioni 5,wananchi na wadau wameshirikiana pia,Je ni lini serikali itatuunga mkono ili kumalizia kituo hiki kwa ajili ya usalama wa wananchi wetu,?”.amehoji.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Daniel Sillo amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2024/2025, serikali imetenga Sh.Bilioni 3.8 kwa ajili ya kumalizia maboma yote 77 yaliyojengwa na wananchi.

“Naomba nimuhakikishie Mh Mbunge baadae tuonane ili tuone pengine kituo chake kipo katika maboma haya hivyo tuweze kumalizia katika mwaka wa fedha wa 2024/2025,”.amesema.

Previous articleWAZIRI MAVUNDE AZINDUA TIMU YA KUANDAA ANDIKO LA VISION 2030
Next articleEWURA YAIBUKA KIDEDEA MIONGONI MWA TAASISI ZINAZOTOA MCHANGO 15% SERIKALINI KWA WAKATI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here