Home LOCAL KIGOMA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

KIGOMA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KWA WINGI UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi wa mkoa wa Kigoma uliofanyika leo tarehe 19 Juni, 2024 katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi wa mkoa wa Kigoma uliofanyika leo tarehe 19 Juni, 2024 katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akizungumza wakati akiwasilisha mada ambapo alisema amesema uboreshaji kwa awamu hii ya kwanza utafanyika kwenye mizunguko 13 na kuongeza kwamba baada ya mkoa wa Kigoma uboreshaji utaendelea kwenye mikoa ya Katavi na Tabora.

 

Wadau wa masuala ya Uchaguzi wakiwa katika mkutano huo Mkoani Kigoma
Viongozi wa Kimila ni miongoni mwa wadau muhimu wa Uchaguzi

Watu wenye ulimemavu nao ni wadau muhimu wa masuala ya uchaguzi, hapa mkalimani wa lugha ya alama akimfanyia tafsri mmoja wa washiriki wa mkutano huo.

Afisa kutoka Idara ya Daftari akiwasilisha mada

 

 

 

 

Washiriki wakichangia mjadala uliofanyika baada ya kuwasilisha mada.
Na. Mwandishi
Wetu, Kigoma

Wananchi mkoani
Kigoma wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao
wakati wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
linalotarajiwa kuzinduliwa mkoani humo tarehe 01 Julai, 2024.

Wito huo
umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa)
Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi wa mkoa wa
Kigoma uliofanyika leo tarehe 19 Juni, 2024 katika Halmashauri ya Kigoma Ujiji.

Jaji
Mwambegele amewapongeza wadau wa uchagizi na wananchi kwa ujumla kwenye mkoa wa
Kigoma kwa mkoa wao kuteuliwa kuwa sehemu ya uzinduzi wa uboreshaji huo ambao
utafanyika kwenye uwanja wa Kawawa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma
Ujiji na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).

“Uboreshaji
wa daftari utazinduliwa hapa mkoani Kigoma tarehe 01 Julai, 2024 na mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa (MB). Tayari Tume imeamua kwamba uzinduzi huo ufanyike katika
uwanja wa Kawawa uliopo hapa kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji,”
amesema Mhe. Mwambegele.

Ameongeza
kuwa Tume ilifikia uamuzi wa kufanya uzinduzi huo kwenye mkoa wa Kigoma baada
ya kuzingatia mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mwamko mkubwa wa
wananchi kujitokeza kwenye uboreshaji wa Daftari uliofanyika mwaka 2019/20.

“Ni matarajio
ya Tume kuwa mtakuwa mabalozi wazuri wa kusambaza taarifa na kuhamasisha
wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili
kuendeleza sifa hii ya mwamko wa wananchi kujitokeza kwa wingi,” amewaambia
wadau hao.

Amesema,
uzinduzi wa uboreshaji wa Daftari utatanguliwa na shughuli mbalimbali za
uhamasishaji ikiwa ni pamoja na matangazo na tamasha la uborshaji wa Daftari
ambalo litafanyika siku ya Ijumaa tarehe 28 Juni, 2024 kwenye uwanja wa Kawawa.

Wakati
akiwasilisha mada, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,
Bw. Kailima, R. K amesema uboreshaji kwa awamu hii ya kwanza utafanyika kwenye
mizunguko 13 na kuongeza kwamba baada ya mkoa wa Kigoma uboreshaji utaendelea
kwenye mikoa ya Katavi na Tabora.

“Zoezi hili
litaendeshwa kwa siku saba kwenye kila kituo cha kuandikisha wapiga kura. Tunatarajia
zoezi litakamilika Machi, 2025,” amesema Bw. Kailima.

Previous articleMAHAKAMA YAKUBALI PINGAMIZI LA EQUITY
Next articleSSERIKALI  KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA UNCDF NA EU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here