Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah Akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Na:Neema Mathew
Morogoro
Wakala wa Usajiri wa Biashara na leseni (BRELA) imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari lengo ni kuwajengea uwezo namna ya kuripoti taarifa zilizo sahihi kwa kutoka kwenye taasisi mpaka kwa Wananchi
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo ambayo yanafanyika Mkoani Morogoro, Juni,18, 2024, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt.Hashil Abdallah, amesema kuwa malengo ya mafunzo hayo ni dhahiri kuwa BRELA imedhamiria kudumisha uhusiano na mawasiliano na wadau muhimu ambavyo ni vyombo vya habari hivyo basi mafunzo hayo yataleta tija,kujua kwa kina majukumu, mafanikio, changamoto na ufumbuzi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi katika utoaji wa huduma bora kwa umma kwa kuzingatia mabadiliko ya teknolojia.
Amesema BRELA imeona umuhimu wa kukaa na wadau muhimu katika kuelimisha na kuhabarisha umma juu ya namna Serikali inavyohudumia wananchi wake kupitia Sekta ya Biashara Kwa kuifahamu BRELA ambayo itarahisisha hata vyombo habari kuwa na uhakika wa taarifa sahihi za BRELA baada ya kupata mafunzo hayo.
“Najua uandishi wa habari unamisingi yake ambayo ninyi wanahabari mnaisimamia pindi mnapokuwa mkitekeleza majukumu kwa ajili ya kuhabarisha umma, Kwenye utekelezaji wa majukumu najua mnajisimamia katika uandishi wa habari pindi mnapofanya kazi zenu za uandishi, mkiongozwa na maadili yanayokubaliwa katika taaluma yenu.
“Niwaombe ndugu zangu wanahabari, kupitia kalamu zenu na vipaza sauti mtusaidie katika kuhakikisha taarifa za BRELA zinatiliwa mkazo ili kuwezesha umma wa Watanzania kwa ujumla kuhamasika katika kurasimisha biashara zao ukizingatia urasimishaji wa biashara hizo zinafanyika kwa njia ya mtandao.
Amesema Zipo changamoto nyingi ambazo wananchi wanakabiliana nazo kwenye hatua ya kufikia urasimishaji wa biashara, ukuaji wa teknolojia huweza kuwa kikwazo lakini hawawezi kusimama wakati dunia inakimbia kutokana na mabadiliko na ukuaji wa teknolojia. Hivyo, changamoto kama hizo waandishi wa habari ndipo taaluma yao inapohitajika katika kuwaelimisha, kuwaelekeza na kuwaongoza umma.
Bw.Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu Brela Akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Amesema Wapo waandishi wa habari wanaweza kuwa na mitazamo tofauti kwa namna wanavyotafsiri sheria za utekelezaji wa majukumu ya BRELA na kupelekea muda mwingine kuandika kichwa cha habari kinachopiga kelele au kichwa cha habari kinachohukumu na kuleta taharuki kwa umma anaamini kupitia mafunzo hayo wataelekezana kwa kina yale ambayo yamekuwa kigugumizi kufuatia tafsiri mbalimbali na kupata majibu ya kina
” Hivyo basi niwaombe nanyi kuwa mabalozi huu usiwe tu kwaajili ya kuelimisha umma bali uanze ndani ya vyombo vyenu vya habari, Vyombo vyenu vinatumia huduma za BRELA ambazo natamani ziwe mfano katika kufanikisha utekelezaji wa huduma za BRELA hasa baada ya kusajili vyombo vyao kama kampuni au majina ya biashara,
BRELA ifanye ziara katia vyombo hivi vya habari na kukutana na wamiliki pamoja na uongozi wa vyombo vyao na hawa washiriki wakiwa ni wenyeji wenu wa kuweza kuwafungulia milango kwa kuwakutanisha na uongozi ili na wao waweze kupewa elimu muhimu na zaidi kuwakumbusha kusimamia utekelezaji wa sheria hasa baada ya Sajili za vyombo vya habari,” amesema Dkt.Abdallah.
‘Kauli mbiu ya mafunzo hayo ni “Vyombo vya habari ni chachu ya ukuzaji Biashara” ambayo yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 21,2024.