Home LOCAL WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUELIMISHA UMMA KUFANYA USAJILI WA BIASHARA ZAO KUPITIA...

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUELIMISHA UMMA KUFANYA USAJILI WA BIASHARA ZAO KUPITIA MFUMO WA MTANDAO

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah, ametoa wito kwa  waandishi wa habari kupitia mafunzo ya Wakala wa usajiri wa Biashara na leseni (BRELA)  kuwa mabalozi wazuri kwa kubeba agenda zitakazoleta mchango chanya hasa kwenye urasimishaji wa biashara ili Wananchi waweze kunufaika na taasisi hiyo
Ameyasema hayo Juni 18,2024 Mkoani Morogoro, wakati wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari yenye lengo la utoaji wa taarifa sahihi zenye  kuelimisha umma juu ya umuhimu wa uhuishaji wa taarifa za kampuni kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao. 
“Tujuavyo serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara hivyo kupitia   Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji, ametoa Notisi ya Msamaha wa asilimia hamsini (50%) ya ada ya uwasilishaji wa nyaraka za kampuni nje ya muda iliyotolewa katika Tangazo la Serikali Na. 410 la tarehe 24 Mei, 2024 na itatumika kwa kipindi cha miezi kumi na mbili tangu kuchapishwa kwake. 
Amesema Waziri ametoa Notisi hiyo kwa kuzingatia kifungu cha 452A cha Sheria ya Kampuni, Sura ya 212 kinachotoa Mamlaka kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya biashara kutoa msamaha wa ulipaji wa ada ya uwasilishaji wa nyaraka za kampuni nje ya muda ,Notisi hiyo imetolewa kwa lengo la kuwezesha uhuishaji wa taarifa za kampuni zilizosajiliwa kabla ya mwaka 2018 kwenye mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandaoni msamaha wa asilimia hamsini (50) unatolewa kwa ada ya ucheleweshaji wa nyaraka 
Amesema Kampuni zilizosajiliwa kabla ya mwaka 2018 ambazo taarifa zake hazijahuishwa kwenye Mfumo wa Usajili wa Kampuni kwa njia ya Mtandao,
Maombi ya kuhuisha taarifa za kampuni yaliyopo kwenye Mfumo wa usajili wa kampuni kwa njia ya Mtandao kabla ya tarehe ya kuchapishwa kwa Notisi hiyo na Maombi ya kuhuisha taarifa za kampuni kwenye Mfumo wa Usajili wa Kampuni kwa njia ya Mtandao yatakayopokelewa kwenye Mtandao ndani ya muda wa Notisi hiyo.
“Msamaha huu uliotolewa, una umuhimu mkubwa sana kwa taifa kwa kuwa utaleta mageuzi makubwa sana kwenye ukuaji wa sekta ya biashara hivyo basi kuna agenda ambazo mnaweza kuzibeba na kuanza kuzifanyia kazi kwa kuzielimisha umma mkiwa kwenye mafunzo kwa hiyo Kila mada mtakayofundishwa ni somo kubwa ambalo litabadili mitazamo ya Wananchi, amesema,” Dkt.Abdallah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here