NA: MWANDISHI WETU.
Kampuni ya dRAFCO GROUP LIMITED imeendesha kampeni ya mafunzo ya Mradi wa Diaper Care iliyofanyika kwenye hospitali ya Mbagala Rangitatu jijini Dar es Salaam tangu Juni 11 mpaka 14, 2024.
Kampeni hiyo ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kuelimisha mama juu ya matumizi sahihi ya taulo (Diapers) za Baby Cheeky,Cuidado na Pinotex,
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi katika kilele cha Mradi huo wa Diaper Care Afisa Rasilimali watu kutoka dRAFCO GROUP Bw. Benjamin Mangi Amesema kwamba mradi huo ulikuwa na lengo kubwa la kuelimisha matumizi sahihi ya Diaper ikiwa ni moja njia mbadala ya wanawake kujiweka safi na kujiepusha na magonjwa na wanapojifungua.
“Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi mzima wa hospitali ya Mbagala Rangitatu pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke pamoja na Mganga Mkuu kwa kukubali kufanya zoezi hili,”amesema.
Pia ameongeza kuwa mradi huo wa Diaper Care lengo lake kubwa ni kuwasaidia wanawake,watoto,watu wakubwa Pamoja na wagonjwa wenye mahitaji maalumu
Amesema kuwa kuanzishwa kwa mradi huo ni moja ya mikakati ambayo wamejiwekea katika kurudisha fadhila kwa jamii ambayo inawazunguka.
Katika hatua nyingine alifafanua kwa wameweza kupata mafanikio makubwa katika utekelezaji wa mradi huo ukiwemo kutoa elimu kwa wahusika pamoja na wasambazaji wa taulo(Diaper) taulo , Cuidado na Cheeky Baby kwa mahitaji mbali mbali.
Ameongeza kwamba wameweza kupata fursa ya kutoa misaada ya moja kwa moja kwa walengwa wakiwemo wakinamama wajawazito,walezi wauguzi,pamoja na watu wenye mahitaji mbali mbali katika hospitali hiyo ya Mbagala Rangitatu.
Amesema mafanikio mengine ambayo wameweza kuyapata katika programu hiyo ni pamoja na kutoa zaidi ya taulo 4500 kwa wahitaji na kutoa elimu kwa watu hao au waangalizi wao wapatao 1055.
Pia aliongeza kuwa wametoa msaada katika hospitali ya Mbagala Rangitatu ambao ni katoni 50 sawa na 7560 za bidhaa mchanganyiko za Baby Cheeky, Cuidado na Pinotex zilizogharimu kiasi cha shilingi milioni 6 kwa ajili ya matumizi ya hospitali ya hivyo kupitia mradi huu wa Diaper Care kampuni ya dRAFCO GROUP imetoa bidhaa mchanganyiko pisi 12.060 zenye thamani ya shilingi 10.575.000.
Benjamin Mangi ameongeza kuwa kwa kutambua umuhimu, uhitaji na manufaa ya taulo hizo kwa wagonjwa na wanawake kampuni ya dRAFCO GROUP inatoa rai kwa serikali na wadau wa afya kutambua umuhimu wa bidhaa hizo na kurahisisha upatikanaji wake ikiwa ni pamoja na kuhimiza umuhimu wa matumizi ya bidhaa hizo.
Ameongeza kuwa kama dRAFCO GROUP tungependa kila begi linalobebwa na mama anapokwenda kujifungua asikose kuweka walau pakiti moja ya taulo hizi za wakubwa kama mbadala wa khanga na pamba ambazo wengi hutumia katika safari yao muhimu ya uzazi
” Tunaomba serikali yetu kwa kushirikiana na mifuko ya bima kuhamasisha upatikanaji wa bidhaa hizi muhimu kwa wagonjwa wote, ” Amesema Benjamin
Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Mbagala rangi tatu Dkt Ally Makori Musa ameishukuru kwa dhati kampuni dRAFCO GROUP kwa kutoa msaada wa mahitaji mbali mbali kwa ajili ya wagonjwa wao.
Amesema kuwa hospitali yao kwa siku ina uwezo wa kupokea zaidi ya wagonjwa zaidi ya 1000 na kati ya hao wakinamama wanaokwenda kujifungua ni kati ya 30 hadi 40 kwa siku.
Mganga huyo amesema ujio wa kampuni hiyo umekuwa ni mkombozi mkubwa kwa upande wao kwani mahitaji waliyotoa ikiwemo taulo ni muhimu sana hasa kwa wakinama.