Home BUSINESS KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KUTOA FEDHA KUENDELEZA MIRADI YA NHC

KAMATI YA BUNGE YAMPONGEZA RAIS SAMIA KUTOA FEDHA KUENDELEZA MIRADI YA NHC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Ahmed Abdallah Ahmed (kulia), akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Tomotheo Mzava, (katikati), na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda, (wa pili kushoto), wakikagua Mradi wa Kawe711, wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua miradi mitatu inayotekelezwa na Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM 

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imempongeza Rais Samia kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kutoa fedha kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwaajili ya kuendeleza miradi iliyokuwa imesimama inayotekelezwa na Shirika hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua miradi mitatu ya Shirika hilo iliyofanyika leo Juni 30,2024 Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Timotheo Mzava, amesema kuwa uamuzi wa Rais Samia kutoa kibali kwa NHC kuendelea na utekelezaji wa miradi yake ni wakizando na kwamba NHC kwa sasa hawana kisingizo cha kutokamilisha miradi hiyo kwa wakati.

“kazi hii isingefanyika vizuri kama siyo nia, moyo, mtazamo na maono ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan hasa kutoa kibali kwa NHC kuendelea na utekelezaji wa miradi hiyo

“NHC kwa sasa hawana kisingizo tena cha kutokamilisha miradi hii kwani tayari fedha zimeshatolewa”amesema Mzava.

Aidha ameipongeza NHC kwa kuonesha umahili mkubwa katika kusimamia na kutekeleza miradi hiyo, nakwamba Kamati imeridhishwa na hatua waliofikia katika utekelezaji wa miradi yake mitatu ikiwemo wa Samia Housing Scheme (SHS), mradi wa Kawe711 na Morocco Square ambayo yote iko Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda amesema kuwa miradi hiyo ipo katika hatua nzuri na kwamba mradi wa Morocco Square umeshakamilika kwa asilimia 99 na tayari majengo yaliyopo yameshachukuliwa na wapangaji na wanunuzi kwa asilimia 90, nakwamba hiyo ni ishara kuwa miradi hiyo sasa inafanya vizuri.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NHC Ahmed Abdallah Ahmed, amsema kuwa hadi sasa katika nyumba za makazi na biashara zilizouzwa,  Shirika limekusanya kiasi cha Sh.Bilioni 30 na kiasi cha Sh.Bilioni 35.9 kinaendelea kukusanywa huku eneo la maduka limeshapangishwa kwa asilimia 98 ambapo kwasasa upangaji wa bidhaa unaendelea ili kufungua maduka hayo mwezi Julai mwaka huu.

Previous articleMWENYEKITI WA CCM Dkt. SAMIA AONGOZA KIKAONI CHA KAMATI KUU (NEC) DODOMA
Next articleSOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 1-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here