Home BUSINESS CBE YAKWAKONGA WAGENI KUTOKA ZANZIBAR 

CBE YAKWAKONGA WAGENI KUTOKA ZANZIBAR 

Na: Mwandishi Wetu, CBE, Dar es Salaam

Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) leo Juni 13, 2024 kimepokea ugeni unaojumuisha Viongozi kutoka Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, kwa lengo la kujifunza na kupata uzoefu wa namna chuo hicho kinavyoendesha shughuli zake.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Chuo, Naibu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Fedha, Mipango na Utawala Prof. Emmanuel Munishi alisema ni jambo la heshima kupata ugeni huo ambao pamoja na kupatiwa maelezo ya kina kuhusu muundo na uendeshaji wa shughuli za Chuo lakini pia wamepata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa chuoni hapo.

“Tunawashukuru sana kuja kututembelea CBE, kwetu imekuwa fursa nzuri ya kuweza kuwasilisha na kutoa uzoefu wa namna Chuo chetu kinavyofanya kazi, ikizingatiwa tuna mpango wa kufungua tawi letu CBE Zanzibar, tunategemea ushirikiano wetu tuliouanzisha leo utaendela kudumu,” alisema Prof. Munishi.

Pamoja na mambo mengine Prof. Munishi alisema Chuo kinatekeleza majukumu yake kwa ushitikiano mkubwa kutoka Wizara mama ya Viwanda na Biashara, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) TCUpamona na vyuo vya jirani hususan katika masuala ya uvumbuzi na ubunifu wa wanafunzi.

Kwa upande wake mwakilishi wa msafara huo ambaye pia ni Mkurugenzi Uendeshaji na Utumishi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar ndugu Suleiman Mohamed Rashid alisema waliamua kufanya zaira hiyo ili kujionea namna Chuo hicho kinavyendesha shughuli zake na kwamba anaushukuru uongozi wa CBE kwani wamepata zaidi ya walichokitarajia.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza Chuo cha CBE kwa namna ambavyo wameweza kuboresha mitaala yao na kuweka mikakati inayoonyesha wamedhamiria chuo hiki kuja kuwa miongoni mwa vyuo bora katika ukanda wa Afrika Mashariki, nimejionea miradi mikubwa ukiwemo mradi wa jengo la zaidi ya Shiling Bill 23 unaoendelea kujengwa pamoja na miundombinu mingi mingine,” alisema Suleiman Mohamed Rashid.

Previous articleMAJALIWA AMKARIBISHA ZUHURA YUNUS OFISI YA WAZIRI MKUU
Next articleDKT.BITEKO AIPONGEZA EWURA UZINDUZI WA TAARIFA YA UTENDAJI WA SEKTA ZA NISHATI NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here