Home BUSINESS BRERA YATOA HUDUMA ZA PAPO KWA HAPO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA...

BRERA YATOA HUDUMA ZA PAPO KWA HAPO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI DAR

Afisa Leseni Kutoka Wakala wa Usajili wa Kampuni na Leseni (BRELA), ask kabidhi cheti cha Usajili kwa mteja aliyefika kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa umma kusajili Biashara yake na kupewa cheti papo kwa hapo, leo Juni 20, 2024 Jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM.

Wakala wa Usajili wa Kampuni na Leseni (BRELA), umeendelea kusogeza huduma zake karibu na wananchi ambapo imeweka Kambi katika viwanja vya Ofisi yake Jijini Dar es Salaam na kutoa huduma za papo kwa hapo kwa wananchi.

Huduma hizo ni sehemu ya shamrashamra za maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Dodoma, ambapo yanatarajiwa kuhitikishwa rasmi Jumaapili Juni 23, 2024.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu yanaongoza na Kauli Mbiu isemayo “KUWEKEZA KWA UTUMISHI WA UMMA WA AFRIKA KARNE YA 21 ILIYO JUMUISHI NA INAYOSTAWI; NI SAFARI YA MAFUNZO NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here