Home LOCAL BRELA KUFANYA USAJILI WA LESENI YA KIWANDA UKIWA POPOTE KUPITIA MTANDAO

BRELA KUFANYA USAJILI WA LESENI YA KIWANDA UKIWA POPOTE KUPITIA MTANDAO

Ili  kurahisisha utoaji huduma Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kupitia mfumo wa kimtandao wa ORS ambao  unaowezesha  kupata huduma zao zikiwemo za kufanya sajili za kibiashara kama leseni ya kiwanda au kusajili ukiwa sehemu yoyote.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Leseni kutoka BRELA, Endrew Mkapa Mkoani Morogoro wakati wa mafunzo ya waandishi wa habari alipokuwa akizungumzia kuhusu Leseni za Viwanda pamoja na usajili ambapo amesema kupitia Mfumo wa mtandao unaweza kupata Leseni au kusajili kiwanda ukiwa mahali kokote
“Mfumo wa kimtandao ambao BRELA tunao tumerahisisha sana katika kupata huduma zetu, hakuna haja ya kuja ofisini maana unaweza kupata usajili wa leseni ya biashara kundi A,kupata leseni ya kiwanda na kusajili kiwanda kidogo kwa kutumia mtandao tu.
Amesema kuwa  viambatanisho ni utambulisho wa mmiliki ambapo atatakiwa kuwa na nyaraka au hati mbalimbali ambazo zinaelezea eneo husika ambalo kiwanda kitakuwepo,uwezo wake kimtaji kwa maana ya uwekezaji na hivyo vyote vitaonekana kupitia andiko na nyaraka nyingine ambazo zitakuwa zimetolewa na taasisi nyingine.
“Viwanda vimegawanyika katika makundi mawili kwa mujibu wa Sheria ambapo kundi la kwanza ni viwanda vikubwa na vya kati ambavyo mtaji wake unaanzia Sh.milioni 100 na kundi la pili linahusisha viwanda vidogo ambavyo mtaji wake uko chini ya Sh.milioni tano na ada ya usajili wa leseni ya kiwanda ni Sh.800,000 na ada hiyo inalipwa mara moja tu kwa uhai wa maisha yote ya kiwanda lakini kwa upande wa Viwanda vidogo ada ya usajili ni Sh.10,000 na hiyo ni kwa muda wote.
“Leseni ya viwanda vikubwa ni Sh.800,000 , halafu kiwanda ambacho uwekezaji wake hauzidi  Sh.milioni ni sh 10,000, uwekezaji ambao unazidi ya Sh.milioni Tano ada yake ni Sh 50,000 na uwekezaji unaozidi Sh.milioni 10 ada yake ni Sh.100,000,”amesema.
Mkapa amesema kuwa baada ya kiwanda kupewa leseni au kusajiliwa kila mwaka wahusika wanatakiwa kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya kiwanda ambapo kuna fomu maalum ya kujaza ambayo inauliza maendeleo ya kiwanda.
“Na hii ripoti ya kiwanda ambayo inatakiwa kuwasilisha BRELA kila mwaka haina malipo katika kiwanda .Ni bure kama ukitoa taarifa ndani ya mwaka lakini ukichelewa ndio kuna faini ndogo kama Sh.10,000.
“Hivyo na BRELA tumejiunganisha na mifumo ya taasisi nyingine lakini mfumo huo una matoleo mengine kwa taasisi inayotaka kuingia katika mfumo wetu ili kurahisisha huduma.Hata hivyo BRELA tumejipanga kuendelea kutoa huduma bora sambamba na kuendelea kurasimisha viwanda,” amesema Mkapa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here