Home BUSINESS BODI YA NHC YAFANYA ZIARA MIRADI YA DAR

BODI YA NHC YAFANYA ZIARA MIRADI YA DAR

DAR ES SALAAM 

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) imefanya ziara katika miradi mbalimbali ya Shirika hilo iliyopo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi.

Ziara hiyo iliyofanyika leo, ilianza saa nne asubuhi na kuwajumuisha wajumbe wote wa Bodi pamoja na viongozi waandamizi wa Shirika.

Katika ziara hiyo, Bodi ilipata fursa ya kutembelea miradi ya Kawe 711, Morocco Square, Samia Housing na eneo la NHC Urafiki ambayo inajumuisha ujenzi wa nyumba za makazi na biashara.

Mwenyekiti wa Bodi, Dk Sophia Kongela, alitoa maelekezo akitaka umuhimu wa kuimarisha utekelezaji wa miradi na kuhakikisha ubora unaendelea kuzingatiwa kwa kila hatua.

“Ni muhimu kwa Bodi yetu kufanya ziara kama hizi ili kujionea moja kwa moja maendeleo ya miradi yetu. Tunajivunia juhudi zinazofanywa na timu yetu ya ujenzi na tunahakikisha kwamba miradi yote inatekelezwa kwa viwango vya kimataifa,” alisema Dk.Kongela.

Viongozi wa NHC waliokuwepo katika ziara hiyo waliweza kutoa maelezo ya kina kuhusu changamoto zinazojitokeza katika ujenzi na hatua ambazo zimechukuliwa ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa.

Bodi inaendelea na ziara katika miradi ya Samia, Morocco Square na Eneo la NHC Urafiki kufuatilia utekelezaji wa maelekezo na miongozo yake.

Ziara hii ni sehemu ya juhudi za NHC katika kuhakikisha kuwa inatoa suluhisho la makazi bora kwa wananchi na kusimamia rasilimali za umma kwa ufanisi na uwazi.

Previous articleNHC KUANZISHA MKOA MPYA WA URAFIKI
Next articleWAZIRI MKUU ATAKA MIPANGO ENDELEVU YA UTAFUTAJI TEKNOLOJIA SEKTA YA MADINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here