Home LOCAL BALOZI NCHIMBI MSIBANI KWA Dkt. NZUNDA

BALOZI NCHIMBI MSIBANI KWA Dkt. NZUNDA

DAR ES SALAAM 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi amejumuika pamoja na waombolezaji wengine, kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Tixon Nzunda, shughuli iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Goba jijini Dar Es Salaam.

Balozi Dk Nchimbi, ambaye alisoma pamoja na marehemu Nzunda Chuo Kikuu Mzumbe, pia aliwapatia pole familia ya marehemu kwa msiba huo, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.

Mwili wa marehemu Nzunda, ambaye alifariki kwa ajali ya gari Juni 18, 2024 huko wilayani Hai, unatarajiwa kuzikwa nyumbani kwao, mkoani Songwe, Juni 22, 2024.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here