Home BUSINESS TANZANIA KINARA AFRIKA KWA USAMBAZAJI WA UMEME KWA WANANCHI

TANZANIA KINARA AFRIKA KWA USAMBAZAJI WA UMEME KWA WANANCHI

Tanzania na Benki ya Dunia kushirikiana katika miradi ya nishati

Benki ya Dunia yaisadia Tanzania dola milioni 300 kuendelea kuimarisha sekta ya nishati nchini

Tanzania yapongezwa kufanya vizuri usambazi wa umeme kwa wananchi

Na: Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Tanzania imepongezwa na Benki ya Dunia kwa kuwa miongoni mwa nchi inayoongoza kusambaza Nishati ya Umeme kwa wananchi wake

Akizungumza leo Juni 4, 2024 ofisini kwake jijini Dodoma, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameishukuru Benki ya Dunia kwa pongezi hizo na kusema kuwa Benki hiyo ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini na kuwa wamekuwa na ajenda ya kushirikiana katika miradi ya nishati.

“Tumefurahi kusikia nchi yetu imepiga hatua na tumejipanga kuendeleza miradi mingine ya nishati ili kuhakikisha kuna utoshelevu wa Nishati hiyo nchini”, amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza “Tutaendelea kushirikiana na Benki ya Dunia na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza kila fedha tunayopata lazima iwe na thamani kwa wananchi. Wizara pamoja na Shirika letu la umeme TANESCO limepongezwa kwa kushughulikia vizuri suala la nishati nchini, hata hivyo ni lazima kuangalia mbali zaidi si tu kuridhika kwa hapa tulipofika.”

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete amesema kuwa Benki hiyo inatambua kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na mfumo mzuri wa kusambaza nishati kwa Watanzania.

“Hapa Afrika, Tanzania ni mfano mzuri katika usambazaji wa Nishati ya Umeme kwa wananchi. Tumejipanga kuwa na mazungumzo zaidi na kuona namna bora zaidi ya kusaidia katika masuala ya nishati safi ya kupikia kwa kufadhili na kuhusisha sekta binafsi kwa kuangalia fursa zilizopo”, amesema Belete.

Aidha, Bw. Belete amesema kuwa Benki hiyo inafadhili pia mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 400 ukutoka Iringa hadi Sumbawanga na kuunganisha nchi za Tanzania na Zambia.

Ameendelea kwa kusema kuwa Benki ya Dunia itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuiendeleza ajenda ya nishati safi ya kupikia ambayo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mwisho.

Previous articleWAZIRI WA FEDHA ALIOMBA BUNGE KUIDHINISHA MAPATO NA MATUMIZI SHILINGI TRIL.18.17
Next articleDkt. NDIEGE AWAALIKA WANAUSHIRIKA MKOANI TABORA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA USHIRIKA DUNIANI 2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here