Home BUSINESS ZOEZI LA UKUSANYAJI MADENI NYUMBA ZA TBA NI ENDELEVU – WAZIRI BASHUNGWA

ZOEZI LA UKUSANYAJI MADENI NYUMBA ZA TBA NI ENDELEVU – WAZIRI BASHUNGWA

Waziri wa Ujenzi, Innocent L. Bashungwa (Mb) akiwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, ambapo atawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/25, Leo tarehe 29 Mei 2024.

………….

Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa ameliambia Bunge kuwa zoezi la ukusanyaji madeni ya kodi za pango kwa wapangaji wa nyumba za TBA ni endelevu, hivyo anatoa wito kwa wapangaji wote kuhakikisha kuwa wanalipa kodi zao kwa wakati kuepusha usumbufu ambao unaweza kujitokeza.

Waziri Bashungwa amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Waziri Bashungwa, ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024, TBA imefanikiwa kukusanya fedha kiasi cha shilingi Bilioni 4.3 kati ya shilingi Bilioni 14.35 ya fedha inazodai kama malimbikizo ya kodi za pango kwa wapangaji katika nyumba zake.

“Mhe. Spika, ukusanyaji wa madeni hayo ni maelekezo ya Bunge lako Tukufu na CAG, hivyo tunawaomba mtuvumilie wakati wa utekelezaji wa zoezi hili kwani ni zoezi endelevu” amesisitiza Waziri Bashungwa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mhe. Selemani Moshi Kakoso ameishauri Serikali kubuni mfumo mpya na rahisi utakaoiwezesha TBA kukusanya madeni na iwapo Taasisi za Serikali na wapangaji wengine watachelewa kulipa, mfumo huo uweze kutoza riba kwa ucheleweshaji.

Aidha, Mhe. Kakoso ameweka wazi kuwa Kamati inasisitiza kuwa TBA iendelee kuchukua hatua kwa kuwaondoa wapangaji ambao taasisi zao zimeshindwa kulipa madeni wanayodaiwa.

Aidha, imesisitizwa kuwa zoezi la ukusanyaji madeni ya kodi za pango la nyumba kwa wapangaji wa TBA ni muhimu, litawezesha TBA kujenga nyumba zaidi kulingana na mahitaji.

Previous articleUJENZI WA VIVUKO BARABARANI KUOKOA VIFO VYA WANAFUNZI JIJINI TANGA 
Next articleUDOM YAGEUKA KIVUTIO MAADHIMISHO YA KITAIFA YA ELIMU,UJUZI NA UBUNIFU TANGA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here