Home BUSINESS TANZANIA NA MAREKANI ZADHAMIRIA KUKUZA BIASHARA

TANZANIA NA MAREKANI ZADHAMIRIA KUKUZA BIASHARA

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah akiongea na waandishi wa Habari, mara baada ya kufungua Mkutano wa siku moja wa majadiliano ya biashara yanatolenga kubaini Ukuaji wa biashara, uliofanyika leo Mei 28,2024 Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Michael Battle wakati akifungua Mkutano wa majadiliano ya biashara yanatolenga kubaini Ukuaji wa biashara, Jijini Dar es Salaam.

DAR ES SALAAM 

Tanzania na Marekani zimedhamiria kuongeza kiwango cha biashara baina ya nchi hizo kutoka kiwango cha Dola milioni 460 zilizofikiwa kuanzia mwaka 2016 hadi 2023.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah akiwa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Michael Battle Mei 28, 2024 Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa majadiliano ya biashara yanatolenga kubaini Ukuaji wa biashara pamoja na kutafuta suluhu ya vikwazo vinavyokwamisha ongezeko la biashara baina ya nchi hizo.

Dkt Abdallah amesema majadiliano hayo yatajikita katika maeneo manne ikiwemo uchumi wa kidigitali, namna ya kufikia masoko, maboresho ya kanuni za udhibiti mazingira ya biashara na ziara ya maonesho biashara.

Ameongeza kuwa majadiliano hayo yanahusisha Wataalam wa nchi hizo mbili ambao wanjadilina namna ya kufikia masoko kupitia mifumo yenye uwazi, kutumia teknolojia ya kidijitali kuleta mageuzi na ukuaji wa uchumi.

Aidha amebainisha kuwa majadiliano yatashugulikia vyanzo vikuu zinavyoathiri utendaji wa makampuni na kukuza mawasiliano na mahusiano ya moja kwa moja kati ya wafanyabiashara wa Marekani na Tanzania

“Majadiliano hayo yanatafsiri kwa vitendo maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika falsafa ya kufungua nchi kibiashara,” alisema Dkt. Abdallah.

Naye Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Michael Battle amesema ushirikiano wa biashara baina ya nchi hizo utasaidia kuongeza ufanyaji biashara baina ya nchi hizo pamoja na kuzifikia fursa mbalimbali zilizopo.

“Marekani ina matumaini makubwa ya kufanya biashara na Tanzania na tunaamini majadiliano yaliyoanza yataweka bayana namna Bora ya ufanyaji biashara baina ya nch hizi,” amesema na kuongeza kuwa “zipo fursa za kushirikiana baina ya nchi hizo na kukuza” amesema Mhe. Battle.

Aidha, aneongeza kuwa Marekani inaiamini Tanzania na kupitia hatua ya majadiliano hayo imedhamiria kukuza kiwango cha ufanyaji biashara haswa kwa kuwa Tanzania ina idadi kubwa ya watu wanaofikia milioni 60.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here