Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko pamoja na Waziri wa Nchi, Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo mara baada ya kuzindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi, Wananchi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kuzindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Maji Nishati na Madini wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Shaib Hassan Kaduara Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri wa Nchi, Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Saidi Jafo Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwenye hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024
DAR ES SALAAMÂ
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suruhu Hassani amezindia Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, huku akiitaka Wizara ya Nishati kukaa na wadau ili kubaini maeneo ambayo yakifanyiwa maboresho yatasaidia upatikanaji wa nishati safi kwa gharama nafuu.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam katika hafla ya Uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, iliyofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Rais Dkt. Samia Suruhu Hassani, amesema kuwa asilimia 90 ya watanzania bado wanatumia Nishati ambayo sio rafiki, huku akisisitiza umuhimu wa kusimamia utekelezaji wa mikakati huo ili kufikia malengo asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi.
Rais Dkt. Samia amesema kuwa wakati umefika kwa sekta binafsi nchini kuongeza uwekezaji na upatikanaji wa nishati safi ya kupikia katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha, Rais Dkt. Samia amewataka kuleta teknolojia rahisi itakayowezesha wananchi kupata nishati safi kadri ya uwezo wao pamoja na kulipia kulingana na matumizi kama inavyofanyika katika umeme.
Rais Samia amesema lengo la Mkakati huo likitekelezwa na kutimia litapunguza gharama ya nishati safi ya kupikia pamoja na kuongeza upatikanaji na uwekezaji wa nishati safi.
Rais Samia amebainisha kuwa Mkakati huo wa kitaifa pia utachangia jitihada za Serikali za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kutokana na uharibifu wa misitu ambao huchangiwa na shughuli za kibinadamu.
Amesema kuwa kwa sasa, inakadiriwa kuwa takribani hekta 469,000 za misitu hupotea kila mwaka ambapo nishati za kuni na mkaa ni moja ya chanzo kikuu cha kutoweka kwa misitu hiyo.
Akisoma taarifa ya Makakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa amesema kuwa mradi huo utagharimu shilling trilioni 4.6 ambao utamudumu kwa muda wa miaka 10 mpaka 2034, huku akifafanua kuwa umefata sera za Kitaifa na Kimataifa ili kuleta tija.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko amesema kuwa lengo la mikakati wa Nishati Safi ya Kupikia ni kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2030 asilimia 80 ya watanzania watumie Nishati Safi pamoja na kusimamia kikamilifu Mkakati huo ili kuleta matokeo ya haraka na kuwawezesha wanawake na vijana kiuchumi.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo, amesema kuwa changamoto iliyopo kwa sasa uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya Taifa ya Nchi, huku akiadi utekelezaji kwa ufanisi.
Wageni pamoja na Wadau mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2024.