Home LOCAL MSD, OSHA WATOA MAFUNZO YA USALAMA KAZINI KWA WATUMISHI

MSD, OSHA WATOA MAFUNZO YA USALAMA KAZINI KWA WATUMISHI

MOROGORO 

Wakala wa Usimamizi wa Afya na Usalama mahala pa kazi (OSHA) kwa kushirikiana na Bohari ya Dawa (MSD) inaendesha mafunzo ya usalama maeneo ya kazi.

Mafunzo haya yanayofanyika mkoani Morogoro kwa siku nne yanatolewa kwa wawakilishi na wasimamizi wa afya na usalama pa kazi wa MSD (MSD Occupational Health and safety, employee representative). Wawakilishi hawa wanatoka kwenye kila Kanda na Makao Makuu ya MSD.

Mafunzo hayo ni utekelezaji wa sheria ya afya na usalama mahali pa kazi namba 5, ya 2003 ambayo inamtaka kila mwajiri nchini kuwa na wawakilishi wa usalama mahala pa kazi ambao wamepatiwa mafunzo ya utoaji huduma hiyo kwa usahihi.

Akifungua mafunzo hayo Mkaguzi wa Usalama wa Mazingira ya kazi Bi. Immaculatha Longino amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa ajili ya kulinda afya za watumishi pindi wanapopata changamoto za kiafya wawapo kazini. _“Watumishi wote walioteuliwa kushiriki mafunzo hayo wanapaswa kuelewa wanachojifunza ili kuwasaidia watumishi wengine maeneo ya kazi”_


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here