Home SPORTS MAGU KINARA MASHINDANO YA UMITASHUMTA MKOA WA MWANZA, YABEBA VIKOMBE 13

MAGU KINARA MASHINDANO YA UMITASHUMTA MKOA WA MWANZA, YABEBA VIKOMBE 13

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani akipokea kombe la mshindi wa kwanza kutoka kwa  Afisa elimu ya awali na msingi wilaya ya Magu Glory Mtui na kukabidhi kombe hilo kwa mkuu wa Wilaya Mh. Joshua Nassri  leo Ijumaa Mei 31/2024 .

Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari akinyanyua kombe la mshindi wa kwanza wa mashindano ya UMITASHUMTA mkoa wa mwanza mara baada ya kupokea hilo leo Ijumaa Mei 31/2024 katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Magu.

Mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi Bujora Mussa Jafari akikabidhi kombe la mshindi wa kwanza mashindano ya ya umoja wa Michezo na taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania (UMITAMSHUMTA) kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mwanza zilizoshiriki mashindano hayo mara baada ya kurejea na ushindi wa vikombe 13 eo Ijumaa Mei 31,2023.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani akiwa katika picha ya pamoja na walimu na makocha waliiongoza kambi ya UMITASHUMTA ya wilaya mara baada ya kurejea na ushindi wa makombe 13 katika mashindano ya ngazi ya mkoa.

Halmashauri ya Wilaya ya Magu imeshika nafasi ya kwanza kimkoa katika Mashindano ya umoja wa Michezo na taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Mshingi Tanzania (UMITASHUMTA) kwa kuchukua vikombe 13 katika fani za mpira wa kikapu wavulana na wasichana, riadha , kwaya, ngoma, mpira wa miguu wavulana, handball , usafi na nidhamu na kombe la mshindi wa jumla katika Halmashauri zote za mkoa wa mwanza zilizoshiriki mashindano hayo.

Akitangaza matokeo hayo mbele ya mkuu wa Wilaya Afisa utamaduni wa Wilaya ya Magu, Peter Mujaya amesema magu imebeba vikombe 13 katika fani ya mpira wa kikapu wavulana na wasichana nafasi ya kwanza, mpira wa mikono wavulana nafasi ya 2, na wasichana nafasi ya tatu, riadha wasichana nafasi ya 1 na wavulana nafasi ya 3, kwaya nafasi ya 1, ngoma nafasi ya 2 , muziki nafasi ya 3, mpira wa miguu nafasi ya 3, usafi na nidhamu nafasi ya 1, mpira wa wavu nafasi ya 3 pamoja na kombe la mshindi wa jumla kwa mkoa wa mwanza.

Akizungumza wakati akipokea vikombe hivyo leo Mkuu wa Wilaya ya Magu Mh. Joshua Nassari amewapongeza vijana  kufanya  vizuri  kwa katika mashindano hayo na akasisitiza kuongeza bidii na kufanya vizuri zaidi katika mashindano  ya Kitaifa.

Aidha DC Nassari ametoa rai kwa wanafunzi hao kutumia ushindi huo katika kuongeza juhudi na bidii katika taaluma na kufanya vizuri katika masomo yao ili kufikia malengo yao na kuifanya wilaya ifanye vizuri katika taaluma.

Naye  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani ametoa pongezi kwa wote waliofanikisha ushindi na kuwataka wafanye vizuri zaidi kwa mashindano mengine hapo mwakani.

Vijana 26 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Magu wameteuliwa kuunda timu ya mkoa itakayoshiriki mashindano ya UMITASHUMTA taifa yatakayofanyika mwezi  Juni  Mkoani Tabora.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here