DAR ES SALAAM
Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wa Kibiashara kati yake na Ufaransa na kukuza teknolojia ya kisasa katika Sekta ya Viwanda.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe kwenye mahojiano na waandishi wa Habari wakati wa Mkutano wa wafanyabiasha kati ya Tanzania na Ufaransa unaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kigahe amesema kuwa mkutano huo unalenga kutoa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili hasa katika kuongeza thamani mazao ya kilimo kwa kuyachakata katika Viwanda vya ndani.
Ameeleza kuwa Tanzania inapeleka bidhaa Ufaransa zinazofikia Dola za Marekani milioni 25122 kwa mwaka, huku Ufaransa ikiingiza bidhaa zenye thamani ya Dola milioni 75.418 Kwa mwaka.
“Katika mkutano huu zaidi ya Kampuni 27 kutoka Ufaransa zimeshiriki, na hii ni fursa kubwa ya kukuza Biashara kwani tunauza kidogo, hivyo tuna kazi kubwa ya kufanya ya kuongeza mauzo yetu ili kutanua wigo wa Biashara na kupata teknolojia mpya za kisasa za viwanda kutoka Ufaransa,” amesema Mhe. Kigahe.
Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchi Tanzania Nabil Hajloud amesema Tanzania ni moja ya nchini zenye utawala Bora na mazingira mazuri ya uwekezaji, na kwamba uwekezaji wa ufaransa ni endelevu na wenye tija.