TUME ya Ushindani (FCC), imesaini mkataba wenye thamani ya sh. Bilioni 1.5 na Trademark Africa kwa lengo la kukuza Uchumi wa Biashara nchini na kuimarisha utendaji kazi wa Tume hiyo.
Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa FCC William Erio, amesema mkataba huo ni wa miaka mitatu, na kwamba ulianza kufanyakazi mwezi Novemba mwaka jana.
Ameeleza kuwa mkataba huo unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili ambapo mwaka moja wataangalia matokeo yaliyopatikana ndani ya miaka hiyo miwili na kujiridhisha utendaji kazi wake kama ilivyokusudiwa.
Aidha, Erio amesema fedha hizo zitatumika katika mambo matatu yakiwemo kufanya maboresho ya miundombinu ya Tehama, mafunzo kwa wafanyakazi wao na kuwekeza zaidi katika mitandao ya kidigitali.
âUnaweza ukawa na miundombinu mizuri, ukawa na kilakitu kilichokamilika lakini kama watumiaji wa mifumo hawaielewi vyema, ufanisi tunaoutarajia hautakuwepo hivyo tutahakikisha wafanyakazi wa FCC wanapata elimu ya kutoshaâ amesema Erio.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Trademark Africa, Elibariki Shammy amesema lengo la kushirikiana na FCC ni kuhakikisha eneo la sera linakuwa bora na kutanua wigo mpana wa biashara ngazi ya kimataifa.
âMkataba huu ni endelevu, kufuatia eneo la sera ya biashara kuwezesha Tanzania kupata fursa ya uwekezaji.
âDunia inakuwa kwa kasi ndiyo maana tumeshirikiana na FCC katika kuhakikisha Tanzania inapiga hatua katika soko la biashara na kuwakaribisha wawekezaji,â amesema Shammy.