MKUU wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex, akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Jerusalem Mbezi Beach, inayomilikwa na Kanisa hilo, leo Mei 11, 2024, Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA HUGHES DUGILO)
DAR ES SALAAMÂ
MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Alex Malasusa, amesema ili kukabiliana na kuharibika kwa maadili, jamii ina jukumu la kushirikiana katika malezi ya watoto yatakayosaidia kuwa na jamii njema kwa ustawi wa familia na Taifa kwa ujumla.
Askofu Dkt. Malasusa ameyasema hayo leo Mei 11, 2024 Jijini Dar es Salaam, katika hafla ya Uzinduzi wa Shule ya Awali na Msingi ya Jerusalem Mbezi Beach, inayomilikwa na Kanisa hilo.
Amesema maadili yanapaswa kujengwa kuanzia ngazi ya chini, na kwamba jambo hilo lazima msingi wake uanzie kwa watoto ambao watayashika na kukua nayo hadi kwenye umri wa uzee wao.
“Maadili hayatokei tu, wala kwenda kuyanunua, bali ni lazima tushirikiane, mimi, na wewe tuungane Îşwenye kurudisha maadili mema kwenye jamii yetu” amesema Dkt. Malasusa.
Ameongeza kuwa Kanisa hilo lilifikia maazimio ya kuanzishwa kwa Shule hiyo, baada ya Mkutano Mkuu wa Dayosisi uliofanyika mapema mwaka huu, na kuamua kuweka mkazo kwenye elimu kwa kuazimka kuanzishwa shule ya awali na Msingi, na kwamba shule hiyo ni ya watu wote bila kujali imani zao, rangi wala kabila.
“Shule hii ni ya watu wote, Shule hii haina ubaguzi na hatutambagua mtu kwa rangi wala Dini yake, kila mtu atapata elimu, kwani Yesu Kristo alikuja Duniani kwaajili ya watu wote”
Kwa Upande wake Mratibu wa Elimu wa Dayosisi ya Dar es Salaam na pwani, Agnes Lema, amesema shule hiyo itakuwa ikitumia mtaala wa elimu ya Dini kwaajili ya kuwajenga watoto katika maadili mema.
“Tumeona bado kuna changamoto ya kukosekana kwa maadili kwa watoto na jamii kwa ujumla, hivyo hapa tutasaidia kumlea mtoto katika maadili mema” amesema.