Home BUSINESS BARRICK ILIVYOADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

BARRICK ILIVYOADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Mfanyakazi bora wa Barrick, Dativa Katabaro, akipokea zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Philip Mpango.
Wafanyakazi wa mgodi wa Barrick waliochaguliwa wafanyakazi bora wakipokea vyeti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Anamringi Macha.

Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu wakishiriki katika maandamano ya Mei Mosi.
Wafanyakazi waliotunukiwa vyeti katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzao.
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu walijumuika na wafanyakazi wenzao kutoka taasisi mbalimbali katika maadhimisho hayo
 
 ***
 
Kampuni ya dhahabu ya Barrick nchini kupitia migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara, iliungana na wafanyakazi wote duniani kuadhimisha siku ya Mei Mosi ambapo wafanyakazi wake walishiriki katika maadhimisho yaliyofanyika katika mikoa ya Arusha,Mara na Shinyanga. 
 
Mkoani Arusha ambapo sherehe hizo zilifanyika kitaifa,mfanyakazi bora wa Barrick Dativa Katabaro ni miongoni mwa wafanyakazi waliotunukiwa vyeti na zawadi na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ambaye alikuwa mgeni rasmi.
 
Mkoani Shinyanga mgodi wa Barrick Bulyanhulu umewapatia vyeti pamoja na fedha taslimu wafanyakazi waliofanya vizuri katika sekta zao wakati shughuli za uzalishaji zikiendelea katika mgodi huo.
 
Kampuni ya Barrick imekuwa na utaratibu wa kutoa motisha za zawadi kwa wafanyakazi wake na kuthamini mchango wao kwenye kampuni.
 
Awali akizungumza mbele ya wafanyakazi na wadau mbalimbali Mgeni rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, aliipongeza kampuni ya Barrick ,kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu unaopatikana Mkoani kwake kwa kuthamini wafanyakazi wake pamoja na kujali maslahi yao pamoja na kuendelea kushirikiana vyema na serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Previous articleBRELA KUADHIMISHA SIKU YA MILIKI UBUNIFU DUNIANI MEI 9, 2024 JIJINI DAR
Next articleWANAFUNZI SAVANNAH PLAINS KUIWAKILISHA TANZANIA MASHINDANO YA UBINGWA WA DUNIA YA KUONGEA KWENYE HADHARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here