Home Uncategorized TUENDELEE KUYAISHI TULIYOJIFUNZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN-MAJALIWA

TUENDELEE KUYAISHI TULIYOJIFUNZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN-MAJALIWA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka waumini wa dini ya kiislam kuendelea kuyaishi yale waliyojifunza wakati Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema kuwa lengo ni kuhakikisha jamii inaendelea kuwa bora na kulifanya Taifa kuwa lenye tulivu, amani na mshikamano “Popote Tanzania unapokwenda utulivu ni mkubwa kwasababu watu wake wanafuata misingi ya dini zao,”

Ametoa wito huo leo (Jumatano Aprili 10, 2024) alipozungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye swala ya Eid iliyofanyika katika msikiti wa Gadaffi jijini Dodoma.

“Viongozi wetu wa dini Mwenyezi Mungu amewapa uwezo wa kuhudumia wanajamii na kuwaeleza yaliyomema, na wameendelea kutoa mchango kwenye Taifa hili ili liendelee kuwa na amani, Mwezi huu tumeona utulivu mkubwa, Mimi niwasihi utulivu huutuendelee nao katika kipindi chote cha miezi kumi na moja iliyobaki mpaka kufikia mwezi Mtukufu mwingine”

Amesema kuwa kila mmoja anapaswa kufuata misingi iliyoimarishwa kwenye jamii zetu ikiwemo kupinga na kukataa ukatili dhidi ya watoto, wanawake na ulawiti

Amesema kuwa Rais Dkt. Samia amekuwa mfano wa kuigwa katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kushiriki ibada ya futari na makundi mbalimbali katika jamii ambayo itawezesha kuijenga jamii yenye misingi imara “Mwaka huu Rais wetu ametuongoza kwenda kwenye maeneo tofauti, tumemuona na watoto wadogo, wazee haya ni mafundisho makubwa yanayotokana na kiongozi wetu”

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amewataka watanzania waendelee kuliombe Taifa ili liendelee kuwa na utulivu na amani “Utulivu wenu watanzania ndio mmefanya nchi hii iendelee kujiamini na kufanya kazi masaa yote bila shida, huu ndio utamaduni mzuri, tuendelee nao”

Previous articleTRAMPA YAZINDUA MAFUNZO MAALUMU KUWAJENGEA UWEZO WATAALAMU WA NYARAKA NA KUMBUKUMBU TANZANIA
Next articleRAIS SAMIA ASHIRIKI KWENYE BARAZA LA EID EL FITRI JIJINI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here