Home BUSINESS TANZANIA COMMERCIAL (TCB) YATOA MIKOPO YA ZAIDI YA BILIONI 700 KWA WASTAAFU

TANZANIA COMMERCIAL (TCB) YATOA MIKOPO YA ZAIDI YA BILIONI 700 KWA WASTAAFU

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Adam Mihayo, akizungumza katika Mkutano wa Taasisi hiyo na Wahariri na waandishi wa Habari uliofanyika leo Aprili 9, 2024 Jijini Dar es Salaam, chini ya Uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Mkurugenzi wa idara ya fedha na mipango wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Bi. Regina Semakafu. akifuatilia wasilisho la Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Adam Mihayo, katika mkutano huo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Anitha Mendoza, katika mkutano huo.

Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabatho Kosuri, akizungumza alipokuwa akitoa neno la utangulizi katika mkutano huo, uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA: Hughes Dugilo)
Na Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM
Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuyafikia makundi mbalimbali katika kutoa huduma zake ambapo hadi sasa wamefanikiwa kutoa mikopo takribani Bilioni 700 kwa wastafu nchini.
Akizungumza katika Mkutano wa Wahariri na waandishi wa Habari uliofanyika leo Aprili 9,2024 Jijini Dar es Salaam,chini ya Uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki  hiyo Adam Mihayo, amesema lengo la kuanzisha mikopo hiyo  ni kuwawezeaha wastaafu kunufaika na kuendelea kustawiaha maisha yao.
Amesema Benki hiyo imeona upo umuhimu wa kutoa mikopo hiyo kwa wastaafu kwani baada ya kumaliza utumishi wao taasisi nyingi za fedha zinawasahau.
“Mpaka sasa tumetoa mikopo takribani Bilioni 700 kwaajili ya kundi hili maalumu ambalo limetumikia nchi.
“Mikopo imekua ikikua mwaka hadi mwaka ambapo mwaka 2023 tumefunga na Bilioni 916 sawa na ukuaji wa asilimia tisa, ambapo mwaka huu mpango mkakati wetu ni kukuza zaidi Sekta ya wafanyabiashara” amesema Mihayo.

Amefafanua kuwa katika kutekeleza mikakati huo wametenga takribani Bilioni 300 kwaajili ya kuwaunga mkono wafanyabiashara ambao wanachangia kwa asilimia thelathini ya ukuaji wa uchumi.
Aidha amefafanua kuwa, Benki hiyo imefanikiwa kuongeza  mapato kutoka Bilioni 43.7 kwenda Bilioni 56.8, nakwamba ongezeko hilo limesababishwa na mapato ya ndani.
“Tunawashukuru wateja wetu kwani wametuwezesha sasa mtaji wetu kukua na kutoa huduma nzuri zaidi” Mihayo amefafanua.
Katika hatua nyingine, Mihayo amezungumzia kuboresha huduma za Kidijitali, ambapo tayari wamefanya mwingiliano na mifumo ya taasisi mbalimbali ikiwemo TRA,GPG,EMS ili kuwawezesha wateja wao kufanya miamala na taasisi za kiserikali.
“Tunafanya utaratibu wa kulipa mishahara kwa wafanyakazi. Kama Kampuni inataka kupitisha mishahara kwetu hiyo huduma tunayo, pia kupitia huduma hiyo tunaweza kutoa mikopo kwa wafanyakazi”,amesema..

Ameongeza kuwa endapo watafanya uwekezaji kwenye maeneo ya kidigitaji, mauzo yataongezeka na kumaliza changamoto ya kutegemea mapato kutoka kwenye riba, na badala yake kukuza mapato yatokanayo na tozo za Biashara.
Kuhusu mtaji, Mihayo amesema kwa mwaka 2023 walifunga na Bilioni 120  na kuishukuru Serikali kwa kuwaongezea mtaji kwani imeonyesha kwamba serikali Ina imani kubwa nao, na hivyo kuahidi kuendelea kuchapa kazi kwa uadilifu.
Ameongeza kuwa kwenye upande wa mapato Mihayo amesema wamekuwa wakiongezeka mwaka hadi mwaka kutokana na taasisi kuaminika, ambapo kwa mwaka jana mapato yalikuwa Bilioni 184.
“Taasisi imekua ikikua mwaka hadi mwaka ambapo mwaka jana amana zimekua kwa takribani asilimia 11 hivyo tunawashukuru wateja wetu kuendelea kutuamini” ameongeza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here