Home LOCAL SERIKALI YATUA RUFUJI, KIBITI KUKUTANA NA WAHANGA WA MAFURIKO

SERIKALI YATUA RUFUJI, KIBITI KUKUTANA NA WAHANGA WA MAFURIKO

Na: Mwandishi Wetu, Maelezo

Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Kisekta wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Muhagama, pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi leo Aprili 10, 2024 wametembelea Wilaya za Rufiji kijiji cha Muhoro na Kibiti kijiji cha Mtunda mkoani Pwani kujionea hali halisi ya mafuriko yaliyoikumba wilaya hiyo pamoja na kuzungumza na wahanga ambao wamekusanyika kwenye vituo mbalimbali baada ya kukosa makazi.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali Mhe. Muhagama aliwasilisha salamu za pole kutoka Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wahanga ambapo pamoja na salam hizo alisema Serikali imelipa uzito suala hilo na ipo kazini kuhakikisha huduma zote muhumu ikiwemo chakula, makazi na madawa vinapatikana katika kipindi hiki ambacho familia hizo zimepoteza makazi.

“Uhai wa wananchi ni jambo la kwanza, tumekuja hapa kuhakikisha tunawapatia huduma zote muhimu katika kipindi hiki ambacho mnakabiliwa na janga la mafuriko, nimeongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri wa kisekta ambao kila mmoja ana timu ya wataalamu tayari wameshaanza kazi, kuna mahitaji muhimu yameshafika na mengine yapo njiani kikiwemo chakula, naomba chakula hicho kitumiwe na wahanga tu, tutafatilia,”alisema Mhe. Mhagama.

Aidha, alitoa rai kwa watendaji kuhakikisha misaada inayopelekwa hususan chakula inawafikia walengwa na kwamba Serikali itafanya ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha pasiwepo watu wasio walengwa kujinufaisha na misaada hiyo ambapo alionya hatua kali zitachukuliwa kwa atakayebainika.

Akiongea katika Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) baada ya ziara hiyo Msemaji Mkuu wa Serikali Bwn. Matinyi, alitolea ufafanuzi wa chanzo cha mafuriko hayo ambapo alisema Serikali ilipokea utabiri kutoka kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), wa kwamba nchi itegemee mvua kubwa za El Nino ambazo zitaungana na mvua za vuli pamoja na masika. Mvua hizo zilianza mwezi Oktoba, 2023 na kwamba taarifa ilitolewa kwa wananchi ili kuchukua taadhari.

“Serikali imetoa maelekezo kadhaa kwa wahanga wa janga hili ikiwemo kuhamia maeneo salama ambapo tayari viwanya elfu 6 vimeshapimwa na vitatolewa bure, vilevile wakazi wa vijiji hivyo wametakiwa kueendelea kuchukua taadhari ili kuepuka matatizo yanayoweza kuambatana na janga la mafuriko ikiwemo kujilinda na mamba wanaotoka mtoni pamoja na kutumia dawa ili kuepuka magonjwa ya mlipuko,” alisema Bw. Matinyi.

Alisema kwa upande wa chakula mpaka sasa tayari mahindi tani 40 yameshapelekwa na unga kiasi cha tani 150 utatolewa, vitu vingine ni maharagwe tani 50 pamoja na mafuta ya kupikia lita elfu 5 vitafikiswa katika maeneo hayo ambayo wahanga wameweka kambi ili kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu.

Mwisho

Previous articleRAIS SAMIA ASHIRIKI KWENYE BARAZA LA EID EL FITRI JIJINI DAR ES SALAAM
Next articlePOLISI, NSSF WAKAMATA WATUHUMIWA 30 KWA KUJIPATIA MALIPO KWA NJIA YA UDANGANYIFU KUTOKA NSSF
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here