Home LOCAL PROF, KABUDI AFUTURISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KILOSA, ASISITIZA AMANI.

PROF, KABUDI AFUTURISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KILOSA, ASISITIZA AMANI.

Na: Yusuph Kayanda

Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof, Palamagamba Kabudi amewataka waumini wa dini Kiislam na dini zengine katika madhehebu tofauti Wilayani Kilosa kulinda misingi ya amani iliyoasisiwa na waasisi wa Taifa la Tanzania kwa kuwataka Wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika shughuli zao ili kuendelea kujenga Uchumi imara wa Taifa.

Akizungumza na mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislam Wilayani Kilosa walioungana pamoja kushiriki katika Iftar iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof, Palamagamba Kabudi katika Msikiti wa Rudewa na kuhudhuliwa na viongozi wa dini mbalimbali akiwemo Shekh Mkuu wa Wilaya Sheikh Nassoro Milambo, amesema misingi ya amani ikiendelea kuasisiwa vyema itajenga jamii bora yenye upendo na kulitumikia Taifa kwa uzalendo.

Prof, Kabudi aliendelea kuwasisitizia waumini wa dini ya Kiislam kuwa Maisha waliokuwa wakiishi katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uliowajenga waumini hao katika mioyo yenye upendo na kuoneana huruma kwa kufturu pamoja, kufanya ibada pamoja ndio Maisha sahihi yenye kukuza Taifa lenye amani, kuheshimiana kwa dini zote ndio misingi itakayowajenga vijana kuwa wazalendo.

Aidha alitumia jukwaa hilo kuwaeleza wananchi juu ya neema kubwa na baraka za Mwenyezi Mungu kwa kuwanusuru wakazi wa Rudewa na janga la mafuriko yaliyotokea Wilayani humo na kuwasihi waendelee kushika Imani za dini ndio ponyo katika Mioyo ya Wanadamu.

Awali akimkaribisha Mbunge huyo, Sheikh Mkuu wa Wilaya Kilosa, Shekh Nassoro Milambo amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananchi wa Kilosa Maendeleo makubwa ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Shule mpya za Sekondari pamoja uboreshaji wa miundombinu ya Mawasiliano.

Sheikh Milambo alisema Maendeleo hayo makubwa kamwe hayajawahi kutokea na kukiri kuwa yanatokana na kumpata Mbunge mwenye kufanya kazi kwa weledi na upendo kwa wananchi wake kwa kuendelea kuchechemua shughuli za kimaendeleo Wilayani humo.

Aidha katika Iftari hiyo Waumini wa dini ya Kiislamu wakiongozwa na Shekh Mkuu wa Wilaya walitumia Fursa hiyo katika kufanya Dua maalumu kwa kuliombea Taifa na Kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliongoza Taifa vyema pamoja na kumtakia Heri Mbunge wao kusimamia vyema Miradi inayotekelezwa jimboni humo itakayosaidia kuchagiza Uchumi kwa Wananchi na Taifa kwa Ujumla.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here