Home BUSINESS ECOPEACE WOMEN INITIATIVE YA SHINYANGA YAPATA MSAADA KUTOKA NVeP KWA UFADHILI WA...

ECOPEACE WOMEN INITIATIVE YA SHINYANGA YAPATA MSAADA KUTOKA NVeP KWA UFADHILI WA BARRICK

Mwakilishi wa shirika la Ecopeace Women Initiative, Anastazia Magembe katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Barrick katika hafla ya kupokea msaada wa dola za Kimarekani 10,000 ambao taasisi hiyo imepatiwa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) kwa kushirikiana na Barrick katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga.
 
Mwakilishi wa shirika la Ecopeace Women Initiative, Anastazia Magembe akifurahia msaada wa dola za Kimarekani 10,000 ambao taasisi hiyo imepatiwa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Shinyanga.
Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Victor Lule (wa nne kutoka kulia) akikabidhi msaada wa wa dola za Kimarekani 10,000 kwa Mwakilishi wa shirika la Ecopeace Women Initiative, Anastazia Magembe katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu.Fedha hizo zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow .Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick.
Kaimu Meneja wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Victor Lule (kulia) akikabidhi msaada wa wa dola za Kimarekani 10,000 kwa mwakilishi wa Mwakilishi wa shirika la Ecopeace Women Initiative, Anastazia Magembe katika hafla iliyofanyika katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu.Fedha hizo zimetolewa na Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP) ) iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow
****
 
Taasisi ya kimataifa ya Nos Vies en Partage (NVeP), kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, imetoa msaada wa dola za kimarekani 10,000 kwa Shirika lisilo la Kiserikali la Ecopeace Women Initiative, lililopo mkoani Shinyanga kwa ajili ya kukabilliana na changamoto za athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazolenga kupunguza wimbi kwa Wanawake na Watoto.
 
Msaada huo umetokana na sehemu ya fedha zilizotolewa na taasisi ya Nos Vies en Partage (NVeP), iliyoanzishwa na inayofadhiliwa na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Barrick Gold Corporation, Mark Bristow, kwa ajili ya kusaidia makundi maalum kama vile Wanawake, watoto na makundi mengine yenye uhitaji yasiofaidika na ukuaji wa kiuchumi barani Afrika.
 
Kila robo ya mwaka taasisi ya NVeP imeweza imeweza kutoa misaada yenye tija na manufaa ya moja kwa moja kwenye jamii zenye uhitaji barani Afrika na kufikia sasa zaidi ya mashirika 15 yasiyo ya Kiserikali na taasisi za kijamii nchini yamepatiwa msaada huo na tayari umeleta mabadiliko chanya katika jamii hususani katika sekta ya elimu, afya kwa Wanawake na watoto na utunzaji wa Mazingira.
 
Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Kaimu Meneja wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Victor Lule, alisema NVeP, itaendelea kusaidia mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanatoa huduma kwa jamii kwendana na malengo ya taasisi hiyo sambamba na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
 
“Tunajivunia kuona fedha zinazotolewa na Barrick kwa kushirikiana na NVeP zinasaidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii kwenye maeneo mbalimbali nchini na tunaamini shirika la Ecopeace Women Initiative, nanyi mtatumia fedha hizi kwa lengo lililokusudiwa” ,alisema Lule.
 
Kwa upande wake Mwakilishi wa shirika la Ecopeace Women Initiative, Anastazia Magembe , ambaye alipokea hundi kwa niaba ya taasisi hiyo , alishukuru kupatiwa msaada huo na alisema kuwa utasaidia kuboresha huduma kwa makundi mbalimbali yenye mahitaji ambayo taasisi hiyo inahudumia, “fedha hizi zinatasaidia kutekeleza programu za utunzaji wa mazingira kwa ajili ya kukabilliana na changamoto za athari za mabadiliko ya tabia nchi zinazolenga kupunguza wimbi kwa Wanawake na Watoto”, alisema Magembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here