Afisa Usajili wa Wakala wa Usajili wa Kampuni na Leseni (BRELA), Ruth Mbaga (kushoto) akitoa elimu kwa mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Abibu Jitwe (kulia), alipofika kupata elimu, katika Banda la taasisi hiyo kwenye maonesho ya Muungano yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Na: Hughes Dugilo. DAR
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), umeendelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea kwenye maonesho ya miaka Sitini (60) ya Muungano wa Tanganyika na Zanizabar, yayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi Aprili 19, mwaka huu, ambapo yamekutanisha taasisi mbalimbali zikiwemo zile za Muungano.
Akizungumza katika Maonesho hayo, Afisa Usajili wa BRELA Ruth Mbaga, amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wananchi kupata elimu juu ya kazi wanazofanya sambamba na kupata huduma za papo kwa hapo ikiwemo usajili wa Kampuni na majina ya Biashara.
BRELA, imekuwa na uhusiano mzuri na Wakala wa Usajili wa Mali na Biashara Zanizabar, (BPRA), katika nyanja mbalimbali ikiwemo usajili wa alama za Biashara na Huduma, pamoja na Hataza.
Pia Kwenye Leseni za Viwanda na Biashara, kwa zile Biashara zenye sura ya Kitaifa na Kimataifa.
Maonesho hayo yamezinduliwa April 19 ambapo yatafungwa rasmi April 25, mwaka huu