Home LOCAL AMEND WARUDISHA TENA MRADI WA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA BODABODA JIJINI...

AMEND WARUDISHA TENA MRADI WA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI KWA BODABODA JIJINI DODOMA

Na: Mwandishi Wetu

BAADA ya kufanyika mafunzo ya elimu ya Usalama barabarani kwa awamu ya kwanza katika Jiji la Dodoma hatimaye mradi huo wa kutoa elimu hiyo tunatarajia kuanza tena lengo likiwa kuwafikia madereva wengi wa bodaboda katika Jiji hilo.

Mafunzo hayo yanatolewa na Shirika la Amend Tanzania kwa kushika na Ubalozi wa Uswisi nchini ambapo awali katika Jiji hilo la Dodoma madereva bodaboda 250 waliopatiwa mafunzo na sasa mradi huo umerejea tena baada ya kutolewa maombi na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri kwamba ni vema mafunzo hayo yakatolewa tena.

Msaidizi wa Miradi kutoka Shirika la Amend, Amiri Matimba amewaambia waandishi wa habari kwamba mafunzo hayo yataanza kutolewa leo Aprili 15, mwaka huu katika kata ambazo hazikupata mafunzo hayo yalipotolewa Februari mwaka huu.

Amefafanua mafunzo hayo yananalenga kuboresha usalama wa waendesha pikipiki, abiria na watumiaji wengine wa barabara, hivyo kuzuia vifo na majeruhi wa matukio ya ajali ambapo wengi wao ni vijana.

Ameongeza kuwa Amend na Ubalozi wa Uswisi wamekubali ombi la mkuu wa wilaya ya Dodoma na kwamba mafunzo yanaanza rasmi April 15 mwaka huu na wadau mbalimbali watashiriki likiwemo Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Wilaya ya Dodoma.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Walimu wa Usalama Barabarani, Mwalimu Massava Ponera amewataka maofisa usafirishaji (bodaboda)kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo ambayo ni muhimu kwa shughuli zao.

“Mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yana umuhimu makubwa kwani mbali na vifo ajali za barabarani husababisha ulemavu wa kudumu huku takwimu za sensa nchini zikionesha kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana na wengi wameamua kujikita katika ujasiriamali wa bodaboda.”

Mwisho

Previous articleCCM TUSIBWETEKE, UCHAGUZI HUU UNA USHINDANI MKUBWA-KINANA
Next articleSOMA HAPA MAGAZETI YA LEO APRILI 16-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here