Home BUSINESS Prof. MKUMBO: Dkt. SAMIA AMELETA SERA JUMUISHI ZA UCHUMI KUKUZA BIASHARA

Prof. MKUMBO: Dkt. SAMIA AMELETA SERA JUMUISHI ZA UCHUMI KUKUZA BIASHARA

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM 

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo (Mb),  amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini, sambamba na kuifungua nchi, ili wafanyabiashara waendelee kunufaika na fursa zilizopo kwa kufanya Biashara zao kwa uhuru ndani na nje ya nchi.

Profesa Mkumbo ameyasema hayo katika hafla ya utoaji Tuzo za Viwanda kwa wanawake wajasiriamali 2024, zilizofanyika usiku wa Mach 16 zilizoandaliwa na Chama cha Wanawake wafanyabiasha Tanzania (TWCC), Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Mheshimwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, muelekeo wa Sera zake katika uchumi, ni ule unaokuwa katika hali jumuishi, unaozalisha ajira na kuleta manufaa kwa wote.

“Katika kuadhimisha miaka mitatu ya Mheshimwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, tunaendelea kueleza sera hizi ambazo Rais wetu amedhamiria kufungua uchumi na kuleta uhuru wa kufanya Biashara” amesema Prof. Mkumbo.

Amewahimiza wanawake kuendelea kuungana katika vyama vyao ili kuzifikia kwa haraka fursa za uchumi, kwani wanawake wengi wana uwezo wa kufanya Biashara na kupambana na viatarishi mbalimbali, na kwamba wanawake hawana sababu ya kuwa wanyonge katika kufanya Biashara.

“Tafiti zinaonyesha kwamba wanawake ni wafanyabiasha bora kuliko wanaume, kutokana na kufanya maandalizi kabla ya kuanza Biashara, na wengi wao wana uwezo wa kuhimili viatarishi vya Biashara kuliko wanaume” amesema Prof. Mkumbo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TWCC Taifa, Bi. Mercy Silla, amesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na mwamko mkubwa wa wanawake kufanya Biashara, na kwamba changamoto kubwa iliyopo ni la urasimishaji wa Biashara zao.

“Tatizo kubwa ni la urasimishaji ukizingatia sasa wakina mama wamekuza Biashara zao kwa kiasi kikubwa hivyo wanahitaji kurasimisha Biashara zao ili waweze kukua” amesema Mercy Silla.

Aidha amesema kuwa TWCC imeliangalia kundi kubwa la vijana na kuwapa nafasi kwa kufungua Soko la vijana kupitia Programu maalum ya vijana ambapo wanapata fursa ya mafunzo ya ujasiriamali na kushiriki katika soko hilo.

“TWCC tumegundua kwamba vijana wetu hawana mahali pakukimbilia, sisi wakina mama tayari tumepiga hatua, sasa tumeliangalia kundi kubwa la vijana, tumewapa nafasi na kufungua soko la vijana” amesema.

TWCC imekuwa ikiandaa halfa ya kuwatambua wazalizaji wa bidhaa za Viwanda kwa kutoa Tuzo kwa waliofanya vizuri, ambapo hii ni mara ya nne mfululizo toka waanzishe Tuzo hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here