Home LOCAL DK. NCHIMBI AWASILI ZIMBABWE MKUTANO WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

DK. NCHIMBI AWASILI ZIMBABWE MKUTANO WA VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akiambatana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya CCM ya Taifa (NEC), amewasili nchini Zimbabwe kushiriki Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika (FLMS), ambao pamoja na masuala mengine utajadili.
Mkutano huo ambao pia utashirikisha watendaji wakuu wa Jumuiya za Wazazi, Wanawake na Vijana wa vyama hivyo, utafanyika kwa siku tatu, kuanzia Machi 17 hadi 20, 2024, katika Mji wa Victoria Falls, kwa ajili ya kujadili agenda mbalimbali zinazohusu urafiki na uhusiano wa vyama hivyo ambavyo vyote viko madarakani, vikiongoza Serikali na Nchi husika.

Katika msafara wake, Katibu Mkuu Balozi Dk. Nchimbi ameambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Komredi Gilbert Kalima, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM), Komredi Fack Raphael Lulandala, na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Zanzibar, Komredi Tunu Juma Kondo.

Mbali ya Chama Cha Mapinduzi, vyama vingine vinavyoshiriki mkutano huo ni pamoja na mwenyeji ZANU – PF (Zimbabwe), MPLA (Angola), SWAPO (Namibia), FRELIMO (Msumbiji), ANC (Afrika Kusini) na Botswana Democratic Party (BDP – cha Botswana).

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, akisalimiana na kuzungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha SWAPO (Namibia), Komredi Mama Sophia Shaningwa walipokutana mara baada ya kuwasili nchini Zimbabwe, leo mchana Machi 17, 2024, kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 11 wa Makatibu Wakuu wa Vyama Marafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, utakaofanyika nchini humo.





Previous articleProf. MKUMBO: Dkt. SAMIA AMELETA SERA JUMUISHI ZA UCHUMI KUKUZA BIASHARA
Next articleHATI 8,325 ZATOLEWA KWA WANANCHI KUPITIA KLINIK YA ARDHI DAR ES SALAAM
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here