Home BUSINESS MIAKA MITATU YA Dkt. SAMIA, TAWA YAPUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI KWENYE MAENEO...

MIAKA MITATU YA Dkt. SAMIA, TAWA YAPUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI KWENYE MAENEO YA HIFADHI

KAMISHNA wa Mamlaka ya Usimamizi a Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda, akiwasilisha mada kuhusu Mafanikio ya TAWA katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mheshimwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichofanyika leo Machi 18,2024 chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabatho Kosuri akiongoza mjadala na maswali kutoka kwa Wahariri na waandishi wa Habari walioudhuria kwenye Kikao kazi hicho.

Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa hilo, Neville Meena, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa hilo.

Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, Anitha Mendoza, (kulia), akiwa na baadhi ya Wahariri wa Habari katika mkutano huo.

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

KAMISHNA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda, amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Mamlaka hiyo imefanikiwa kupunguza  migogoro ya mipaka ya ardhi kati ya Hifadhi na wananchi.

Kamishna Nyanda ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mafanikio ya TAWA katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mheshimwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichofanyika leo Machi 18,2024, chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jijini Dar es Salaam.

Amesema TAWA imeendelea kushirikiana na wananchi katika kutatua migogoro kwenye maeneo ya hifadhi kwa kutekeleza maelekezo ya Serikali yaliyotolewa kupitia Kamati ya Mawaziri nane (8) wa Wizara za Kisekta. 

“Kwa kushirikiana na wananchi migogoro mipaka katika Mapori ya Akiba saba (7) ya Swagaswaga, Mkungunero, Wamimbiki, Igombe, Liparamba, Mpanga Kipengere na Selous kati ya nane (8) yaliyotolewa maelekezo na Kamati ya Mawaziri nane wa kisekta imemalizika ambapo jumla ya vigingi 1,681 vimesimikwa kuzunguka mipaka ya hifadhi” amesema Kamishna Nyanda.

Aidha, amesema kuwa katika utatuzi wa migogoro hiyo eneo lenye ekari 103,544.48  limemegwa  kutoka kwenye hifadhi  na kuwapatia wananchi kwa ajili ya shughuli za kiuchumi, na kwamba Serikali kupitia TAWA inaendelea kukamilisha zoezi la kulipa fidia kaya 145 zilizo katika Pori la Akiba Mkungunero.

Ameongeza kuwa Mamlaka hiyo imekuwa na mipango ya muda marefu katika ya matumizi ya ardhi katika kutatua changamoto hiyo.

“Tuna kazi kubwa ya kufanya kwenye maeneo hayo ili kuokoa maisha ya watu wasidhurike na wanyama wakali na waharibifu” ameongeza.

Kamishna Nyanda amebainisha mikakati iliyochukuliwa na TAWA, katika utatuzi wa migogoro hiyo, ambapo eneo la ekari 103,544.48 limetengwa kutoka kwenye hifadhi, na kuwapatia wananchi kwaajili ya shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF, na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa hilo, Neville Meena, amesema kikao kazi hicho kimekuwa na manufaa kwa Wahariri na waandishi wa Habari kujifunza na kufahamu kazi mbalimbali za Mamlaka hiyo, huku akiwashauri waandishi kuendelea kujifunza kwa kusoma taarifa mbalimbali za Mamlaka hiyo ili kuwa na wigo mpana wa kuifahamu Taasisi hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here