TMDA
Home LOCAL KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA WODI YA WANAWAKE...

KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA WODI YA WANAWAKE HOSPITALI YA WILAYA KIGAMBONI 

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, imewashika mkono akinamama wilayani Kigamboni kwa kutoa vifaa tiba kwenye hospitali ya wilaya hiyo.

Vifaa hivyo tiba hivyo ni pamoja na viti mwendo na vifaa vya kupima presha vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5 kwa wodi ya wanawake ya hospitali hiyo iliyopo Kibugumo, Kigamboni, Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Fatma Abdallah akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba hivyo ikiwa sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, leo Machi, 8, 2024, alisema Puma Energy inaamini vifaa vilivyo kabidhiwa vitaleta ahueni kwa jamii.

“Machi 8, ya kila mwaka imekuwa ikiadhimishwa Siku ya Wanawake Duniani, tumeona tusikae nyuma, hivyo tumejumuika na wenzetu kuadhimisha siku hii kitofauti. Tumeona tuguse jamii, na jamii yenyewe ni inayotuzunguka.

“Puma tumekuja kukabidhii vifaa tiba katika wodi ya wanawake katika Hospitali ya Wilaya ya Kigamboni, tumejitahidi kukusanya vifaa tiba kadhaa vyenye thamani ya Sh. milioni 6.5. Tunavyo vifaa tiba mbalimbali kama viti mwendo na mashine za kupima presha, tunaamini vitasaidia katika wodi ya wanawake. Tunafamu wodi ya akinamama ni eneo lenye changamoto nyingi na wagonjwa wengi.

“Hivyo kunahitajika uangalizi tofauti, sio kwamba tunajipendelea sisi wanawake lakini wodi ya wanawake inahitaji uangalizi wa tofauti kidogo,” amesema Fatma.

Amefafanua Puma kuna wanawake zaidi ya 48 na hatua kubwa imepigwa kaunzia mwaka 2023 kwani wakati anaingia Puma mwaka jana kulikuwa na wafanyakazi wanawake asilimia 9 lakini sasa hivi imefika asilimia 16 huku akisisitiza wanawake wengi wameingizwa kwenye uongozi.

Hata hivyo amesema wanaendelea kutengeneza mazingira kuwawezesha, kuwathaminisha na kuwaleta pamoja wanawaje ili waweze kuleta maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

“Puma tutaendelea kusaidia sekta ya afya kama tulivyosema, tunaangalia sekta ya afya na sekta ya elimu,”amesema huku akikumbusha kuhusu Puma ni kwamba ni kampuni kubwa inayojuhusisha na sekta ya mafuta , ni kampuni ambayo inawabia wawili.

“Sisi tunaongoza katika soko la mafuta lakini bado tunaendelea kukua , tunaimani maono yetu ni kuhakikisha tunafikia wananchi wengi ambao hawapati huduma ya mafuta kwa ukaribu.

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi Matroni Eva Sambaya amesema wanashukuru kupatiwa vifaa hivyo na Puma imeonesha kuwathamini na kuwajali kwani ziko hospitali nyingi katika jiji la Dar es Salaam.

“Katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani Puma mmeona haja ya kuja kwetu na kutushika mkono , vifaa hivi kwetu vitasaidia katika kutoa huduma katika wodi ya wanawake.”

Wakati huo huo Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni(DMO) Dk.Lucas Ngamtwa amesema wanatoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Puma kwa namna ambavyo wameguswa na kuamua kuwashika mkono katika hospitali hiyo.

“Hospitali yetu ni mpya bado tunachangamoto nyingi ikiwemo ya watalaam na vifaa tiba lakini kwa kutambua hilo Kampuni ya Puma mmeona mje mtushike mkono kwa kuhakikisha akina mama wanaokuja kupata huduma katika hospitali yetu wanakuwa salama na wanajifungua katika mazingira mazuri.”

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YAKABIDHI VIFAA TIBA KATIKA WODI YA WANAWAKE HOSPITALI YA WILAYA KIGAMBONI