Home LOCAL KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YARIDHISHWA...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UWEKEZAJI WA MITAJI YA UMMA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI NA MIRADI YA NYUMBA (NHC)

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC)
imeridhishwa na utekelezaji na usimamizi wa miradi ya Nyumba wa Kawe 711, Samia Housing Schem, Morocco Square inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Akizungumza leo Machi 20, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) walipotembelea miradi ya NHC, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Deus Sangu, amesema kuwa kamati yake imeridhishwa na utekelezaji wa miradi baada ya kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na

NHC.

Mhe. Sangu amesema kuwa miongoni mwa majukumu yao ni kuangalia mitaji ya umma ambayo imewekezwa na serikali katika taasisi zake.

Amesema kuwa NHC ni moja ya Mashirika ya kimkakati ambapo serikali imekuwa ikiwekeza fedha nyingi na mpaka kufikia mwaka wa fedha uliyoisha serikali tayari imewekeza shilingi trilioni 5.14.

“Shirika lina miradi mingi, leo tumetembelea miradi iliyopo Mkoa wa Dar es Salaam ambayo Kawe 711, Samia Housing Schem pamoja na Morocco Square” amesema Mhe. Sangu.

Amefafanua kuwa mradi wa Kawe 711 ni mradi wa kimkakati ambapo serikali imewekeza shilingi bilioni 143 ambao utekelezaji wake upo asilimia 25 na utaratibu kumaliza mwezi Aprili 2026.

Ameeleza kuwa mradi wa Samia Housing Schem una thamani ya shilingi bilioni 48 ambapo nyumba zote 560 tayari zimenunuliwa.

Amesema kuwa mradi wa Morocco Square una thamani ya shillingi bilioni 137 na tayari umemilika kwa asilimia 98.

“Kamati tunapongeza kwa kazi kubwa iliyofanywa na NHC katika kusimamia na kutekeleza miradi hii kwa ufanisi mkubwa” amesema Mhe. Sangu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Hamad Abdallah, ameishukuru kama kwa ushauri ambao wamekuwa wakitoa katika kuhakikisha Shirika linapiga hatua.

Amesema kamati imefanya kazi kubwa katika kuzungumza Shirika Bungeni na kufikia malengo tarajiwa, huku akisisiza kuwa mradi wa Morocco Square unatarajia kuanza kufanya kazi hivi karibuni.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here