Home LOCAL JESHI LA POLISI MOROGORO LAMTIA MBARONI ANAYETUHUMIWA KUMUUA MKEWE

JESHI LA POLISI MOROGORO LAMTIA MBARONI ANAYETUHUMIWA KUMUUA MKEWE

MOROGORO.

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro  linamshikilia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la  Mohamedi Omari  mkazi wa kijiji cha Kimamba A wilayani  Kilosa  kwa tuhuma za  kumuua mkewe  na kumzika ndani ya chumba chao.

Mohamedi Omari mkazi wa kijiji cha Kimamba A  wilayani Kilosa mkoani Morogoro anatihuiwa kumuua mkewe kisha kumzika ndani ya chumba wanacho lala.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema baada ya kufanya mahojiano na watoto wa mama huyo aliyetambulika kwa jina la Beatrice Haiyasi wameeleza jinsi walivyopitia unyanyasaji mpaka kupelekea kukosa huduma muhimu za kielimu kutokana na kufungiwa ndani.

Pia ameeleza kuwa tukio hilo limebainika mara baada ya mtuhumiwa huyo kudaiwa kuuza mabati ya mkewe, ndipo kukukatokea ugomvi hikuw watoto wa marehemu wakimsihi mama huyo kuacha kugombana na Baba yao kwani anaweza kumuua kama alivyofanya kwa mama yao.

“Tulipata taarifa za mama huyu kuuawa na mume wake kutoka kwa wasamaria wema hii ni baada ya kutokea ugomvi kati ya mtuhumiwa na mke wake wa sasa ndipo watoto wa marehemu wakaanza kumkanya mama huyo kuwa asigombane na mtuhumiwa huyo kwani atauawa kama alivyomuua mama “ alisema Shaka.

Kwa upande wao majirani wameeleza kuwa familia hiyo ilikuwa ni ngeni katika eneo hilo na kwamba  hawakuwa wakichangamana  na wakazi wa eneo hilo kwani walikuwa ni watu wa kujifungua ndani.

Nae Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama amesema tayari wamemshikilia mtuhumiwa huyo kwa uchunguzi zaidi na ukikamika atafikishwa Mahakamani.

Previous articleKICKSTART YAENDESHA KONGAMANO LA WADAU WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI SHINYANGA
Next articlePATA HABARI MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 23-2024
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here