Home LOCAL FOMU YA URAIS NI MOJA 

FOMU YA URAIS NI MOJA 

Dar-es-Salaam Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongoza uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kumuwezesha Rais Dkt. Samia kuchukua fomu ya kugombea Urais mwaka 2025 ambapo tukio hilo limefanyika Machi 10 2024 na ameongoza wanawake kuchanga fedha kwa ajili ya kumchukulia fomu 

Fedha hizo zimechangwa wakati wa mkutano wa Wanawake wa kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa Kinara wa Nishati Safi ya kupikia, Mazingira na Afya ya Mama na Mtoto.

Fedha hizo kiasi cha  zaidi ya Shilingi Milioni 120 zimekabidhiwa kwa Waziri Mkuu na Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum Mhe. Doroth Gwajima kwa niaba ya wanawake hao.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here