Home LOCAL FCS YAPATA MKURUGENZI MPYA, KUANZA KAZI RASMI MEI 1,2024

FCS YAPATA MKURUGENZI MPYA, KUANZA KAZI RASMI MEI 1,2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society FCS, anayemaliza muda wake wa uongozi Bw. Francis Kiwanga (kulia), akimkabidhi nyaraka za Ofisi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo, Justice Rutenge (kushoto), katika hafla fupi ya makabidhiano ya uongozi wa Taasisi hiyo, iliyofanyika Machi 5, 2024 Jijini Dar es Salaam. (Katikati), ni Mwenyekiti wa Bodi ya FCS Bw. Ali Laai.

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS anayemaliza muda wake wa uongozi Francis Kiwanga akizungumza muda mfupi kabla ya kukabidhi nyaraka za Ofisi na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo Justice Rutenge. Hafla hiyo imefanyika leo Machi 5,2024 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa bodi ya FCS, DKt. Ally Laay, (kulia), akizungumza alipokuwa akielezea mchakato mzima wa kumpata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo. (Kushoto), ni Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge.

Baadhi ya Waandishi wa Habari na watumishi wa FCS wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Ally Laay muda mfupi kabla ya kufanyika makabidhiano ya nyaraka za Ofisi kati ya Francis Kiwanga, Mkurugenzi Mtendaji anayemaliza muda wake, na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi hiyo, Justice Rutenge.

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM 

Mkurugenzi Mtendaji wa FCS anayemaliza muda wake wa uongozi Francis Kiwanga, amesema Shirika la Asasi za Kiraia nchini (FCS) linajivunia miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuheshimu na kusimamia misingi ya demokrasia.

Kiwanga amesema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya uongozi kati yake na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge aliyechaguliwa hivi karibuni.

Amesema kuwa FCS inajivunia uongozi wa Rais Samia unaoheshimu misingi ya democrasia na uhuru wa watu, ambapo amebainisha kuwa FCS itaendelea kuwa daraja kati ya watu na serikali katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

“Kwetu sisi tunaona ni taasisi inayopigania misingi ya utawala bora, tunahitaji kuendeleza juhudi za kupambania maendeleo ya watu, na hili ni suala la kujikumbusha kila siku” amesema Kiwanga.

Aidha, ameongeza licha ya kuwa anamaliza muda wake amehahidi kuendeleza ushiriano na Shirika hilo na atakuwa balozi kwa kutoa mchango wake pindi atakapohitajika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi à Mkurugenzi Mtendaji mpya, bodi imemwamini kuwa atafanya kazi vizuri na kuendelea aliposhia kiwanga kutokana na sifa alizo nazo na ni kijana” amesema Laay.

Naye Mkurugenzi Mtendaji mpya wa FCS Justice Rutenge, ameahidi kufanya kazi kwa weledi kulingana na taaluma na ujuzi alio nao kwa maslahi mapana ya jamii na serikali kwa ujumla.

Previous articleBARRICK BULYANHULU NA KAKOLA DIGITAL SOLUTION WAGAWA MICHE YA MITI KATIKA SHULE YA MSINGI BULYANHULU MSALALA
Next articleCUBA NA TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here