Home LOCAL DIB YATANGAZA NEEMA KWA WALIOKUWA WATEJA WA BENKI YA WANANCHI MERU

DIB YATANGAZA NEEMA KWA WALIOKUWA WATEJA WA BENKI YA WANANCHI MERU

:Mhasibu Mwandamizi wa DIB Silvani Makole akiwasilisha mada kuhusu Ufilisi wa Benki ya Wananchi Meru mbele ya wafanyakazi pamoja na viongozi wa vijiji wa Wilaya ya Arumeru.

Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Arumeru Dkt Amani Sanga akifungua rasmi mafunzo ya DIB kwa wafanyakazi na viongozi wa vijiji mbalimbali wa Halmashauri ya Meru.

Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana Nkanwa Magina akiwasilisha mada.

Wafanyakazi wa Halmashauri na Viongoxi wa vijiji wakifuatilia mada.

Mwenyekiti wa Kamati ya kuongoza waliokuwa na amana katika Benki ya Wananchi Meru Godwin Nderingo akitoa neno la shukuran baada ya mafunzo.

Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa DIB Joyce Shala akimuelimisha mfanyabiashara na mteja wa zamani wa benki ya Meru wakiwa soko la Leganga – Usa river.

Wakufunzi wa DIB wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kutoa elimu kwa Wakilima wa kijiji cha King’ori

DIB walitoa elimu kwa umma kwa kupitia redio maarufu ya Safina FM Arusha, pichani Meneja Uendeshaji Nkanwa Magina (kushoto) na Mhasibu Mwandamizi Silvani Makole wakitoa mada.

Elimu sokoni Tengeru ikiendelea

,…………………. 

Bodi ya Bima ya Amana imetangaza kwamba wale wote waliokuwa wateja katika Benki ya Wananchi Meru (Meru Community Bank) ambao hawajachukua amana zao zilizokuwa chini ya Shilingi 1,500,000 wafike katika tawi la Benki ya Biashara ya Tanzania (TCB) tawi la Meru au Tawi la Benki Kuu Arusha kwa ajili ya kurudishiwa amana zao.

Hayo yalisemwa na Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana, Nkanwa Magina wakati wa mfululizo wa mafunzo kuhusiana na Uwepo wa DIB, Majukumu ya DIB na Mfumo wa DIB, mafunzo yakielekezwa kwa makundi mbalimbali wilayani Meru hususani kwa viongozi wa Vijiji, Wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali,

Wafanyabiashara kwenye minada na masoko mbalimbali ya wazi ambayo yapo katika vitongozji vya King’ori, Kikatiti, Maji ya Chai, Usa River na Leganga. Mafunzo hayo yalidumu kwa wiki nzima na kuhitimishwa leo.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Dkt Amani Sanga aliishuku DIB kwa kuleta elimu hio katika muda muafaka kwani wananchi wengi waliopo katika wilaya ya Meru walikuwa wamekata tamaa ya kuhifadhi fedha zao katika taasisi za fedha baada ya kuanguka kwa benki waliokuwa wanaitumainia na kuipenda ya ‘Meru Community Bank.“Mimi nikiwa mmoja wa wahanga waliopoteza fedha zao baada ya kufungwa kwa benki yetu ya Meru, najisikia fahari leo hii kusikia kwamba hatimae sasa ninaweza kwenda kupewa amana yangu katika tawi la benki ya TCB”.

Aliwaasa wananchi wote kuziamini taasisi za fedha ambazo zina leseni ya Benki Kuu ya Tanzania kwa sababu amana zao zinalindwa na Bodi ya Bima ya Amana.

Naye kiongozi wa Kamati Teule ya Kusimamia Ufilisi upande wa Waliokuwa Wateja wa Benki ya Wananchi Meru Godwin Nderingo aliwapongeza DIB kwa kufanya kazi yao kwa waledi mkubwa ili kuwahakikishia wananchi wanapata haki zao.

“Ingawa muda umekuwa mrefu sasa yapata miaka 6 tokea kufungwa kwa benki hii na zoezi la ufilisi likiwa limefikia asilimia 70, ni ushauri wetu sisi tuliokuwa wateja kuwaomba watu wote waliokuwa wanadaiwa na benki hii kurudisha fedha walizokopa ili zoezi hili lifikie mwisho”.

Wakati wote wa mafuzno wananchi walifurahia zawadi mbalimbali zilizokuwa zilizotolewa wakati wa mafunzo ikiwa ni pamoja na majibu ya maswali yao yaliyokuwa yakijibiwa kwa umahiri na wakufunzi wasaidizi Joyce Shala na Sylvani Makole.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here