TIMU ya Azam FC imefanikiwa kutibuka mshindi kwa kuichapa timu ya Yanga SCtoka nyuma na mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Katika mtanange huo uliopigwa katika Dimba la Benjamín Mkapa Jijini Dar es Salaam ulikuwa wa ushindani ambapo timu zote zilicheza kwa kushambuliana.
Bao la Yanga lilipachikwa kambani na mshambuliaji wake Clement Mzize katika dakika ya 10 ya mchezo huo, kabla ya Azam FC kutokea nyuma kwa ambapo Azam FC walisawazisha dakika ya 19 likifungwa na Gibrill Sillah na kwenda mapumziko wakiwa sare
kipindi cha pili Azam FC walipata goli la pili kupitia kwa kiungo mshambuliaji Feisal Salum Abdallah dakika ya 51 ya mchezo huo.
Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 47 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na Yanga ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Vigogo wengine katika mbio za ubingwa, Simba SC wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 45 wakiwa tayari wamecheza michezo 19.