Home LOCAL WADAIWA SUGU HUDUMA ZA MAJI KORTINI

WADAIWA SUGU HUDUMA ZA MAJI KORTINI

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa muda wa siku 30 kwa wateja wenye malimbikizo ya muda mrefu wa bili za maji kulipa kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kuwafungulia mashtaka.

Afisa biashara Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mlandizi Ndugu, Salome Stephano ameyasema hayo wakati akizungumza na wadaiwa hao na kusema kuwa Mamlaka inawataka wateja wenye malimbikizo ya muda mrefu mrefu wa zaidi ya siku 30 kujitahidi kulipa madeni yao mapema ndani ya muda kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa.

Ameongeza kuwa pamekuwepo na wateja sugu wa muda mrefu wanaolimbikiza madeni yao kufikia miezi mitatu ambao na kutokana na hilo Mamlaka imewashtaki katika vyombo vya sheria.

“Mamlaka imefikia uamuzi wa kuwapeleka wadaiwa sugu Mahakamani kutokana na kulimbikiza madeni kwa muda mrefu licha ya kukumbushwa mara kwa mara kulipa, Mamlaka imewataka kulila bili zao na pia kwa wenye mkataba kuendelea kupunguza madeni yao kwa utaratibu uliowekwa na DAWASA ili kuondoa usumbufu wa mara kwa mara,” ameeleza.

Lustic Paul mkazi wa Mtaa wa Mtongani amesema amekiri kuwa na deni la huduma za maji na kuahidi kulipa ndani ya muda uliopangwa.

Amewasihi wateja wengine wenye malimbikizo ya muda mrefu kulipa ili kuisaidia Mamlaka kuendelea kufikisha huduma ya maji kwa maeneo mengine yasiyokuwa na huduma.

Mkoa wa kihuduma DAWASA Mlandizi inahudumia jumla ya kata 11 ambazo ni Kwala, Mlandizi, Mtambani Visiga, Mbwawa, Kawawa, Janga, Kilangalanga, Ruvu, Vigwaza na Mtongani.

Previous articleTANZANIA, POLAND ZAJADILIANA FURSA ZA KIUCHUMI 
Next articleDKT. SHELUKINDO AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA KAMATI YA SIASA NA DIPLOMASIA YA SADC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here