MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake(UWT) Mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Mbwambo ametoa rai kwa wanafunzi wa sekondari ya Yusufu Makamba iliyopo wilayani Ubungo kuhakikisha wanajikita katika masomo na kuachana na kujikita katika makundi yasiyofaa.
Ametoa rai hiyo kwa wanafunzi hao wakati akitoa mafunzo maalum kwa vijana hao yaliyohusu masuala mbalimbali yakiwemo kuwahimiza kusoma ba kuzingatia maadili yaliyomema hasa kwa kuzingatia Taifa linawategemea katika siku chache zijazo.
Mafunzo hayo yanakwenda sambamba na maadhimisho ya siku kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM)ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam Chama hicho kimekuwa kikifanya shughuli mbalimbali katika jamii.
“Ni Muda wa kujitazama na kuangalia nini kimetuleta shule na kuacha mambo ya makundi ambayo yanaharibu maisha yetu ya baadae hivyo ni muda wa kila mmoja kujiandaa kutengeneza kesho yake njema”
Mbwambo ameweka wazi kuwa Sekondari ya Yusufu Makamba ni moja ya shule ambazo zinatajwa kwa kuwa na wanafunzi wenye tabia chafu hivyo amewataka sasa kubadilika.
Pia ametoa pongezi kwa walimu wa shule hiyo kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kulea kundi hilo ambalo ndio watanzania na viongozi wa baadae.