Home BUSINESS KIGAHE AONGOZA UJUMBE WA wa TANZANIA KATIKA MKUTANO WA SCTIFI – EAC

KIGAHE AONGOZA UJUMBE WA wa TANZANIA KATIKA MKUTANO WA SCTIFI – EAC

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (wapili kutoka kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (wapili kutoka kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi (wakwanza kutoka kulia) wakiimba wimbo wa Afrika Mashariki wakati wa wakishiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo DRC na Sudani Kusini kilichofanyika jijini Arusha tarehe 09 Februari 2024.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) kilichofanyika jijini Arusha tarehe 09 Februari 2024.

Mkutano huo ulijumuisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo DRC na Sudani kusini uliongozwa na Südani Kusini kama Mwenyekiti.

Ujumbe wa Tanzania ulijumuisha wajumbe kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara(TANTRADE), Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Tume ya Ushindani (FCC) na Mamlaka ya Mauzo ya Bidhaa Nje ya Nchi.

Previous articleNCHI WANACHAMA WA EAC ZAKUBALIANA KUINGIA JUMUIYA ZA KITANDA NA KIMATAIFA KWA PAMOJA 
Next articleMSD YATUNUKIWA TUZO KATIKA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MAGONJWA YA MOYO 
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here