Home BUSINESS KATIBU MKUU UWEKEZAJI AKUTANA NA MKUU WA MASUALA YA KIUCHUMI EU JIJINI...

KATIBU MKUU UWEKEZAJI AKUTANA NA MKUU WA MASUALA YA KIUCHUMI EU JIJINI DAR

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida leo tarehe 15 Februari, 2023 jijini Dar es salaam amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Idara ya masuala ya Kiuchumi (Head of Governance and Economic Section) kutoka Umoja wa Ulaya (EU) Bi. Karina Dzialowska na kujadiliana kuhusu namna wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kuibua mikakati mbalimbali inayolenga kuongeza uwekezaji nchini.

Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kiuchumi, Bi. Karina alimhakikishia Dkt.Kida kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Aidha, Bi. Karina alibainisha uwepo wa fursa ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uwekezaji katika miradi rafiki kwa mazingira (Green investment) ambayo itatokana na fedha zinazopatikana kupitia Masoko ya mitaji kwa Amana mahsusi kwa ajili ya miradi rafiki kwa mazingira (Green Bonds).

Vilevile, katika kikao hicho viongozi hao wamezungumzia utekelezaji wa Mpango wa Maboresho ya mazingira ya Biashara na Uwekezaji BLUEPRINT unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Business Environment Growth Innovation (BEGIN)

Previous articlePROFESA  MSAMBICHAKA  AKIPIGIA CHAPUO NEEC
Next articleSERIKALI YAELEKEZA MAAFISA MASUULI KUTENGA FEDHA ZA UKAGUZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here