TMDA
Home LOCAL KATIBU MKUU CCM ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO MSIBA WA BALOZI LUTENI JENERALI...

KATIBU MKUU CCM ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO MSIBA WA BALOZI LUTENI JENERALI MWAKALINDI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akitia saini kitabu cha maombolezo wakati wa kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali (mstaafu) Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile, katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, jijini Dar Es Salaam, Februari 2, 2024.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akisalimiana na Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi (majenerali wastaafu) nchini, wakati wa shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali (mstaafu) Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile, iliyofanyika Ijumaa, Februari 2, 2024, katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, jijini Dar Es Salaam, kuanzia kushoto ni Jenerali Robert Mboma, Jenerali George Waitara, Jenerali Davis Mwamnyange na mwishoni kulia ni Jenerali Venance Mabeyo na nyuma yake ni Ndugu Abbas Mtemvu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam (mwenye kofia).

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Stergomena Lawrence Tax (Mb), wakati wa shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali (mstaafu) Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile, iliyofanyika Ijumaa, Februari 2, 2024, katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, jijini Dar Es Salaam. Katikati yao ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Jacob John Mkunda.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwapatia mkono wa pole familia ya Luteni Jenerali (mstaafu) Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile wakati wa shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali Mwakalindile, iliyofanyika katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, jijini Dar Es Salaam, Ijumaa Februari 2, 2024. Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akitoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali (mstaafu) Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile, katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo, jijini Dar Es Salaam, Ijumaa Februari 2, 2024.


Rais Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Jacob John Mkunda wakati kiongozi huyo alipoongoza waombolezaji wengine kushiriki shughuli ya kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa marehemu Luteni Jenerali (mstaafu), Balozi Martin Nikusubula Mwakalindile, iliyofanyika Hospitali Kuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), leo Ijumaa, Februari 2, 2024. Kulia katika picha ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Stergomena Lawrence Tax na kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea KATIBU MKUU CCM ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO MSIBA WA BALOZI LUTENI JENERALI MWAKALINDI