Home LOCAL KANISA ANGLIKANA MASASI LATENGA ZAIDI YA BILIONI 1.4 KUPELEKA HUDUMA YA MAJI SAFI...

KANISA ANGLIKANA MASASI LATENGA ZAIDI YA BILIONI 1.4 KUPELEKA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI 10  MTAMA

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi George Mbilinyi kushoto,akimsikiliza mhandisi wa maji wa Kanisa la Anglikana Doyasisi ya Masasi Olaph John kuhusiana na ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na Doyasisi hiyo katika vijiji kumi vya Halmashauri ya  wilaya Mtama.

Afisa usafi wa mazingira wa kanisa la Anglikana Doyasisi ya Masasi George Mgaza, akitoa taarifa zinazochukuliwa kabla na wakati wa ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa na kanisa hilo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama mkoani Lindi George Mbilinyi kulia, wakati wa ziara ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya Mtama kutembelea utekelezaji wa miradi ya maji.

Baadhi ya wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya wilaya Mtama mkoani Lindi,wakimsikiliza Mhandisi wa maji wa kanisa la Anglikana Doyasisi ya Masasi Olaph John walipotembelea mradi wa maji wa Mandwanga unaotekelezwa na kanisa hilo kwa gharama ya zaidi ya Sh.milioni 400.

Na: Mwandishi maalum, Mtama

WANANCHI wa vijiji kumi vya kata ya Mandwanga na Mnara katika Halmashauri ya wilaya Mtama mkoani Lindi,watanarajia kuondokana na changamoto ya huduma ya maji safi na salama katika maeneo yao.

Ni baada ya Kanisa la Anglikana Doyasisi ya Masasi kuanza ujenzi wa miradi mitano ya maji  itakayogharimu zaidi ya Sh.bilioni 1.4  ambayo itakapokamilika itamaliza  changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa vijiji hivyo.

Katibu Mtendaji wa Doyasisi hiyo Joyce Liundi alisema,ujenzi wa miradi hiyo ni  katika kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita ya kutatua changamoto ya maji na  kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.

Liundi amevitaja vijiji vinavyokwenda kunufaika na miradi hiyo ni Malungo, Mnazimmoja, Nyundo 1,Nambahu, Chiuta,Mikongi Mandwanga,Lindwandwa vilivyopo kata ya Mandwanga na Mkanga 11 na Chikombe kata Mnara.

Ameishukuru serikali kwa kuwaunga mkono katika utekelezaji wa miradi hiyo na wananchi  wa vijiji hivyo kwa kukubali kutoa maeneo yao bure hali iliyowezesha kutekeleza miradi  bila  ya vikwazo vyovyote.

Aidha,ametoa wito kwa wananchi wa vijiji vilivyopata miradi hiyo kuhakikisha wanatunza maeneo yaliyopitiwa na miradi,kulinda miundombinu na vifaa vinavyoletwa kwa ajili ya  ujenzi ili waweze kunufaika na miradi hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mtama George Mbilinyi,amelishukuru Kanisa la Anglikana Doyasisi ya Masasi kuunga mkono jitihada za serikali kwa kujenga miradi ya maji katika vijiji ambavyo kwa muda mrefu havina huduma ya maji ya bomba.

Alisema,miradi hiyo inayotekelezwa chini ya ufadhili wa kanisa la Anglikana inakwenda kutimiza adhima ya serikali ya kufikisha huduma ya maji kwa wananchi wa Halmashauri hiyo umbali usiozidi mita 400 kutoka kwenye makazi yao na kumtua mama ndoo kichwani.

Mbilinyi,ameagiza kuongezwa nguvu kazi katika ujenzi wa miradi hiyo ili ikamilike haraka na wananchi waanza kupata huduma ya maji safi na salama kwenye makazi yao.

Amewataka wananchi wa vijiji hivyo, kuhakikisha wanatunza miradi hiyo inayojengwa mahususi ili kuwapunguzia muda wa kutembea umbali mrefu na kutumia muda mwingi  kwenda kutafuta maji muda ambao wangeweza kuutumia katika shughuli nyingine za maendeleo.

Aidha,amewapongeza wananchi waliokubali kutoa maeneo yao ili kupisha ujenzi wa miradi ya maji ambapo amewaomba kuendelea kushirikiana na serikali na wadau wa maendelea katika kutatua baadhi ya changamoto zilizopo katika maeneo yao.

Awali Mhandisi wa maji wa Doyasisi hiyo Olaph John alisema,katika awamu ya kwanza miradi inayotekelezwa ni mitano  ambayo ni mradi wa maji Nambahu- Nyundo 1,Chiuta-Mikongi na Mandwanga-Lindwandwali.

Alisema,miradi hiyo ilitarajia kukamilika mwezi Februari mwaka huu, lakini walishindwa kukamilisha kwa muda uliopangwa kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo mvua kubwa zinazoendelea kunyesha,hata hivyo itakamilika mwishoni mwa mwezi Machi.

Kwa mujibu wa Olaph ni kwamba,miradi mingine miwili ya Mnazimmoja-Malungo na Mkanga 11-Chikombe ambayo tayari imefanyiwa upembuzi itaanza kutekelezwa haraka iwezekavyo  ili wananchi wa vijiji hivyo  ili wapate huduma ya maji safi na salama.

Kaimu afisa mtendaji wa kata ya Mandwanga Aletu Kambona alisema,  adha ya maj safi na salama katika  kata hiyo ni kubwa na kwa sasa wananchi wanalazimika kutumia maji ya mito na vyanzo vingine vya asili ambavyo maji yake siyo safi na salama.

MWISHO.
Previous articleUJENZI WA BWAWA LA KIDUNDA WASHIKA KASI
Next articleNMB,YANGA WAZINDUA KADI MAALUM ZA WANACHAMA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Open chat
GREEN WAVES MEDIA
Ahsante kwa kutembeiea KANISA ANGLIKANA MASASI LATENGA ZAIDI YA BILIONI 1.4 KUPELEKA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJI 10  MTAMA