Home BUSINESS GGML YAZINDUA MPANGO WA MAFUNZO KAZINI KWA MWAKA 2024/2025, WANAFUNZI 40 KUFAIDIKA

GGML YAZINDUA MPANGO WA MAFUNZO KAZINI KWA MWAKA 2024/2025, WANAFUNZI 40 KUFAIDIKA

KATIKA kudhihirisha dhamira ya kuwajengea wahitimu wa vyuo mbalimbali kukubalika kwenye soko la ajira, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imezindua mafunzo tarajali kwa wanafunzi 40 waliohitimu vyuo mbalimbali nchini.

Mafunzo hayo yanayotolewa kwa muda wa mwaka mmoja (2024/2025), yatahusisha programu mbalimbali ikiwamo za uanagenzi, mafundi mchundo, watalaam wa masuala ya madini ya fani nyingine ambazo zimeanzishwa ili kukuza ujuzi wa vijana wa kitanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo Makamu Rais Mwandamizi – Kitengo cha Biashara Afrika, Terry Strong amesema mpango wa mafunzo hayo huwapa wahitimu wasio na ajira nafasi ya kupata uzoefu wa kazi ambao unakamilisha masomo yao na unaweza kuwasaidia kushindana katika soko la ajira.

Akiwakaribisha wanafunzi hao 40 waliofaulu usaili ili kuanza rasmi mafunzo hayo chini ya udhamini kamili wa GGML, Terry alisema mpango huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2009, umenufaisha jumla ya wahitimu 258 (pamoja na waliopo sasa) kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu nchini Tanzania.

Terry pia ameakaribisha wahitimu 10 wa mafunzo hayo kwa mwaka jana ambao wamepatiwa ajira za kudumu ndani ya GGML. 

“Walengwa ni 41% ya Wanawake na 59% ya wahitimu wa kiume. Kati ya wahitimu 258 walioandikishwa, 34% (87) waliajiriwa na GGML kwa mkataba wa kudumu katika nafasi mbalimbali ndani ya kampuni, huku wengine wakiajiriwa kwa mkataba wa muda.

“Kwa kuzingatia mafanikio kadhaa yaliyofikiwa hadi sasa, GGML imejitolea kuendelea na mpango wa mafunzo kazini kama mpango muhimu wa kuajiri,’ alisema. 

Alisema mpango huo umetumika kama chanzo kikuu cha wahitimu kuing’arisha GGML kwa vipaji walivyojaliwa na kuwatayarisha wahitimu kutekeleza majukumu muhimu ndani ya kampuni kwa muda mfupi, wa kati na mrefu na kutoa mfano kuwa waliomaliza mwaka jana 10, wamepatiwa ajira za kudumu ndani ya GGML.

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela mbali na kuishukuru GGML kwa kutekeleza mpango huo, pia alilipongeza kundi hilo la wahitimu wa vyuo mbalimbali wanaobahatika kupata mafunzo GGML kwa mwaka huu 2024/2025.

“Kitendo cha kupata fursa hii ndani ya GGML, sio njia tu ya kupata uzoefu, lakini ni chachu ya kutambua uwezo wako kwa ukamilifu. Kabiliana na changamoto, tumia maarifa yako na uruhusu shauku yako ikupeleke kwenye ubora,’ alisema.

Wakati huo huo Mkuu wa Idara ya Mafunzo na Ujuzi, Albert Rukeisa akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri (ATE), Suzanne Ndomba – Doran aliipongeza GGML kwa jitihada zake ambazo kwa zaidi ya miaka 15 zimekuwa chachu kwa waajiri wengine kuendelea kutoa nafasi kwa vijana kujifunza na kuongeza wataalam wa madini katika sekta hiyo.

Pia amewapongeza wanafunzi hao walipata fursa ya kujiunga na mafunzo hayo kwa vitendo kwa mwaka 2024/2025.

“Sanjari na hilo nipende kutoa rai kwa vijana hawa, waswahili wanasema “Ukishikwa shikamana” Nendeni mkaweke bidii ya kazi, uaminifu, mkizingatia usalama na taratibu zote za mgodi nanyi mtayaona mema ya utii na bidi katika kujifunza kazi,” amesema.

Aidha, mmoja wa wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo mwaka jana na kupata bahati ya kuajiriwa ndani ya GGML, Diana Laswai, mbali na kuishukuru GGML pia waliishukuru Serikali kwa kuendelea kuhamasisha sekta binafsi kutoa mafunzo kazini kwa vitendo.

Ametoa mwito kwa wanafunzi wapya wanaoanza mafunzo hayo mwaka huu  kufanya kazi kwa bidii, kuzingatia nidhamu na kuzingatia tunu za GGML ambavyo ni usalama.

Naye Grace Msafiri ambaye ni mmoja wa wanafunzi waliopata fursa ya mafunzo hayo kwa mwaka huu, pia aliishukuru GGML kwa kuwapatia fursa na kuwawekea mazingira rafikin ya kazi.

Aidha, ameahidi kutumia mafunzo hayo kwa kufanya kazi kwa bidii ili waweze kufika mbali ili na wao wapate fursa za kuajiriwa katika maeneo mbalimbali pindi watakapohitimu.

Previous articleMHE. KAIRUKI AZINDUA MKAKATI WA KITAIFA WA MIANZI, AWATAKA WADAU KUSHIRIKI KIKAMILIFU
Next articleDkt. NCHIMBI ATUA KAGERA, MAZISHI YA BALOZI DK. DIODORUS KAMALA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here