Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekutana na viongozi wa Serikali, Kata na kamati za Wilaya ya Kigamboni na kutoa elimu ya utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira.
Akizungumza na viongozi hao , Afisa maendeleo ya jamii DAWASA, Vivian Silayo ameeleza umuhimu wa kuwepo na kamati hizi pindi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inapoanza na kuziomba kamati kuwa na weledi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
“Kamati hizi husaidia utatuzi wa changamoto wakati wa utekelezaji wa miradi, hii husaidia miradi kukamilika kwa wakati na kutokwama, niwatake kamati zote kufanya kazi karibu na wananchi na kuhakikisha changamoto zinafikishwa sehemu husika kutatuliwa kuendana na miongozo iliyopo” ameeleza ndugu Silayo.
Silayo ameongeza kuwa maoni, na mependekezo yote yaliyotolewa na kamati hizi katika miradi iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa inafanyiwa kazi kwa wakati na kuhakikisha huduma bora inaifikia jamanii.
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Kigamboni Mhe. Stephano Warioba ameeleza kuwa kamati hizi zimekua msaada kwa jamii kwani husaidia miradi kutekelezwa kwa haraka na wepesi na pale inapotokea changamoto basi hutatuliwa kwa utaratibu mzuri, huku akitoa wito kwa DAWASA kuongeza wigo wa wataalamu wanaounda kamati hizi.
Jumla ya kata 7 na mitaa 14 Katika kutoa elimu juu ya utatuzi wa changamoto zinazojitokeza kipindi cha utekelezaji wa miradi zoezi lililoenda sambamba na kupokea ripoti, maoni na ushauri katika miradi iliyokamilika.