Home LOCAL WAZIRI MAKAMBA ATETA NA MKURUGENZI MKUU IOM

WAZIRI MAKAMBA ATETA NA MKURUGENZI MKUU IOM

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Uhamiaji (IOM) Bi. Amy Pope jijini Roma, Italia.

Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Makamba ameipongeza IOM kwa kazi inazofanya nchini katika masuala ya Uhamiaji na amemuhakikishia Bi. Pope kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kufanya kazi na Shirika hilo kwa ukaribu zaidi.

Mhe. Waziri Makamba amesema Shirika hilo limekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya wakimbizi, majanga ya asili na kwamba ni matumaini yake kuwa Tanzania na IOM zitaendelea kushirikiana kwa manufaa ya pande zote mbili.

Waziri Makamba ameipongeza IOM kwa kuendelea na zoezi la kuwarejesha nyumbani raia wa Ethiopia waliokuwa katika magereza mbalimbali nchini na kuongeza kuwa kitendo hicho kimesaidia Tanzania kukabiliana na changamoto ya msongamano wa watu katika magereza yake.

Kwa upande wake, Bi. Pope ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa jinsi inavyoshirikiana na Shirika la IOM katika kutekeleza majukumu yake na kuahidi kuwa na mpango maalum wa kuendeleza ushirikiano na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha majukumu yake. Aliongeza kuwa Shirika hilo litahakikisha kuwa wahamiaji wanapata haki zao za msingi na kuwa katika mazingira salama nchini.

Previous articleMELI 13 ZINAHUDUMIWA MUDA HUU BANDARI YA DSM JANUARI 28/2024
Next articleORYX YAKABIDHI MITUNGI YA GESI NA MAJIKO YAKE 700 KISARAWE,KUFUNGA MFUMO WA GESI MINAKI SEKONDARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here