Home SPORTS SIMBYA SC YAIZIDI MUNG’AA

SIMBYA SC YAIZIDI MUNG’AA

TIMU ya Wekundu wa Msimamizi Simba SC  imeichapa timu ya Singida Fontain Gate mabao 2-0 katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliopigwa katika Dimba la Amani Complex Mjini Zanizabar.

Magoli yote ya timu ya Simba yamepatikana kipindi cha pili cha mchezo huo yakifungwa na Willy Onana katika dakika ya 47 na goli la pili lilifungwa na Luis Miquison dakika ya 59 ya mchezo huo.

Hadi filimbi ya mwisho timu ya Simba imetoka kifua mbele kwa ushindi mnono Katika mtanange huo.

Nahodha wa timu ya Simba SC katika mchezo huo Shomari Kapombe amezungumzia mchezo huo muda mfupi baada ya kumalizika.

“Mchezo ulukuwa mzuri, kipindi cha kwanza Singida walikuwa Wazuri sana na kushika Dimba, lakini maelekezo ya mwalimu katika kipindi cha pili yaliiwezsha timu yetu kufanya vizuri zaidi na kuibuka mshindi” amesema Kapombe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here