Home LOCAL SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII NA KUSHIRIKIANA NA WADAU...

SERIKALI KUENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA USTAWI WA JAMII NA KUSHIRIKIANA NA WADAU WENGINE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wageni, viongozi mbalimbali pamoja na Washarika wa Kanisa la Azania Front wakati wa Ibada Maalum ya Kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa iliyofanyika Kanisani hapo Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Januari, 2024.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi zawadi ya picha Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa mara baada ya kuingizwa kazini wakati wa Ibada Maalum iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa mara baada ya Ibada Maalum ya Kumuingiza kazini Askofu huyo iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front Jijini Dar es Salaam tarehe 21 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuimarisha huduma za ustawi wa jamii na kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha huduma hizo zinapatikana.

Rais Samia amesema hayo leo wakati wa hafla ya kuingizwa kazini kwa Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) iliyofanyika Kanisa Kuu la Azania Front.

Aidha, Rais Samia amesema taasisi za dini zina mchango mkubwa katika kuwajenga waumini kiimani na kujenga taifa lenye watu wema, wanaowajibika katika jamii na kuwa wastahmilivu zinapotokea changamoto.

Vile vile, Rais Samia amesema ni muhimu kuimarisha taasisi ya familia kwani ikiwa imara na yenye masikilizano, itatoa malezi mema kwa mtoto na itaandaa muumini, mwanajamii na raia mwema.

Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhama na kuzingatia tahadhari zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini ili kuepuka athari zinazotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.Rais Samia pia ameitaka Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kufuatilia kwa karibu changamoto zinazojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini ambayo yameathiriwa na mvua hizo.

Hali kadhalika, Rais Samia ameziagiza pia Wizara za kisekta zikiwemo Wizara ya Maji, Nishati, na Ujenzi kuwa kwenye hali ya tahadhari na kujipanga kutoa msaada kwa haraka katika maeneo yanayokumbwa na athari za mvua.

Zuhura YunusMkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here